Kati ya Watanzania Milioni 64, Maprofesa ni 226 tu. Baba wa Taifa ndiyo wa kubeba hii aibu

Mkuu 😊🤓 inabidi uikane nafasi yako ukiwa mzee wa kula kimasiala au unataka kuanzisha familia mapema au ukiwa mzee wa ku copy & paste sikuizi Kuna untpliagalism software so unatakiwa uwe una acknowledge nukuu za kazi za wengine 🤣🤣🤓🤓

After PHD Ili mtu awe PROFESSOR at least ni safari ya hata miaka 10 na zaidi maana Huyu mtu awe anafanya tafiti na utafiti wake uweze ku be PUBLISHED AT INTERNATIONAL JOURNAL
Akifikisha machapisho kumi ambayo yote yata be published in INTERNATIONAL JOURNAL
ndio Huyu mtu aweze kua professor so sio lelemama 🤓🤓
 
Hiyo oroodha wamo kina Profesa Mruma,Ndarichako,Mkumbo na wengine wa type zao?kumbe bado tatizo ni kubwa
 
Ww hujielew kuwa professor halaf huna impact ni bora usiwe.
 
Na hii comment ni kigezo kingine kwamba Tz tuna wajinga wengi sana.
Mjinga ni wewe, tungekua tunajuana tungepimana kwa uwezo wa kufikiri ktk kutafuta mafanikio kimaisha na nione una nini na nina nini, nyie ni wajinga tu
 
Nyerere ndio amelilostisha hili Taifa,sijui Huwa mnamtetea Kwa lipi? 25 years madarakani lakini hakuna kitu Cha maana
Wewe na miaka uliyonayo umefanya nini cha maana kwa mchango wa taifa? Hakuna andiko wala IPR yoyote unayomiliki.

JKN amefanya part yake. Kuunganisha watu wa makabila mbalimbali na kuleta umoja wa kitaifa inatosha kwa yeye kukumbukwa.
 
And do they have any impact for the betterment of MAMA TZ !!??
 
Umemaliza chuo na diploma yake huna ajira uwende ukasome bachelor au masters ya nn ndio maana maprofessor ni wa chache.
 
Samahani, nimechelewa kuona uzi lakini nauliza yule aliyeokotwa jalalani yupo hapo kwenye hesabu yako?

Kama yupo mtoe, hesabu ni 225.

Hao wakenya unaosifia, nimeona juzi prof mmoja wa geology anahojiwa BBC kuelezea kitaalamu tetemeko la Morocco linawezaje kutokea. Maelezo yake yametawaliwa na neno I don't know na kigugumizi kingi
 
Usitafute excuses kia huyo prof.1 wa Kenya.

Kwa Hali hii ya dropout , maprofesa watatoka wapi?

View: https://www.instagram.com/p/CxKacsPMf3_/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==
 
JKN amefanya part yake. Kuunganisha watu wa makabila mbalimbali na kuleta umoja wa kitaifa inatosha kwa yeye kukumbukwa.
Muunganiko huu huu ambao bado wazanzibari na watanganyika wanaitana machogo na mayahee wala urojo? Achalia mbali hilo, makabila tu ya bara ndo yanaanza sasa kuingiliana kwa kumeza tofauti zao za kimila na desturi baina ya kabila moja na jengine! na hii imesababishwa zaidi na ukuaji wa miji ya kibiashara na wala sio jitihada maalumu za kuyaunganisha haya makabila.

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, sifa yake kubwa mi nadhani ni kusimamia lugha ya kiswahili kuwa ndo lugha rasmi ya taifa, japo hili pia limekuja na gharama ya kufifiisha elimu kiujumla kwa ile hali ya elimu yetu kuwa kama ampicilin (rangi mbili) primary kiswahili na secondary kingereza. Hii imepelekea wanafunzi wengi kushindwa kujifunza sawasawa wanapoingia sekondari kutokana na kukosa misingi ya lugha hiyo kule primary, matokeo yake tumekuwa na wahitimu wengi lakini wenye ushindani mdogo wa kitaaluma (na hapa wala siongelei application ya walichosoma bali ni understanding tu ya hizo theory walizosoma)

Ila ukweli utabakia kuwa matatizo yetu kama nchi yanaendelea kukua siku hadi siku kutokana na maamuzi ya muundo wa kikatiba na mifumo ya utawala ambayo huenda maamuzi mengi katika hayo yalifanywa kwa sababu za kisiasa ama kulinda utawala wa awamu ya kwanza kutoka kwa waliokuwa wapinzani wa utawala huo.

I stand to be corrected.
 
Sasa mkuu kama wewe na familia Yako mlikua hamuoni umuhimu wa kusoma kufikia kiwango Cha PhD tatizo ni nani , Familia yenu au nyerere ?

Naona tumeamua kubebesha lawama watu wengine hata Kwa mambo ambayo tulipaswa kuwajibika sisi
 
Sasa mbona Tanzania imejaa wajuaji sana?wakifika 500 si moto utawaka?
 

Kenya Kesho kutwa tunawapita kiuchumi pamoja na ma professor wao!! Unafikiri uchumi unaendeshwa na ma professor??
 
Hivi unahisi kuwa na maprofesa wengi ndo nn?maprofesa wenyewe hawa wa KUSHUKURU KUOKOTWA JALALANI?

Ila kwa ukiritimba wa Tz...hii hali hata usiishangae...kubaniana kwingiiiiiii!%
 
Nilidhani wale wajamaa watamtetea mwalimu kama wanavyowatetea akina kiduku,putin....kumbe unafiki tu wa ki agenda fulani!
 
Katika hao maprofesa umewahesabu Kalamaganda Kabugi? Umemuhesabu Mruma aliyeendeshwa Kama gari bovu na watoto wa kizungu?
Umemuhesabu Osoro?
 
Naomba kufahamu tofauti kati ya associate proffesor na full proffessor!
Tofauti yao ni ranking. Unaanzia Tutorial Assistant, ukipata masters unakuwa Assistant Lecturer, ukifanya publications kwa miaka mitatu au ukipata PhD unakuwa na raking ya Lecturer. Ukishapata ranking ya lecturer unaweza kuandika machapisho, vitabu au research ndani ya miaka mitatu unaomba usenior lecturer. Sasa kutoka usenior lecturer ukifanikiwa kuchapisha Tena na kuleta manufaaa kwenye jamii na international recognition unapewa u associate professor. Baada ya u associate professor utafanyiwa review baada ya miaka mitano Kama upewe full proffesor.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…