Kati ya wifi za mitandao ya simu (Airtel, vodacom) na wifi za kujitegemea TP-Link etc

Umkonto umsizwe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2023
Posts
454
Reaction score
949
Habari members,

Naomba kuuliza jambo Moja ambalo linanichanganya pia sijaelewa kuhusu aina za hizi wi-fi mfano wi-fi za vodacom na za TP-Link Zina utofauti gani pia na cost zake za kila mwezi mwenye details naomba msaada
 
Habari members,

Naomba kuuliza jambo Moja ambalo linanichanganya pia sijaelewa kuhusu aina za hizi wi-fi mfano wi-fi za vodacom na za TP-Link Zina utofauti gani pia na cost zake za kila mwezi mwenye details naomba msaada
Router ni kifaa tu Cha kutengeneza wifi hakiuzi bando, bando unanunua toka kwenye line Yako, so utumie router ya Voda ama ya Tp link haitabadilisha gharama.

Router za kina Voda ndio hizo hizo za Huawei, Zte, D-Link, TP-Link na wengine wanabadili tu brand.

So we angalia menu ya kifurushi unga unachokimudu hizo router zisikuumize kichwa.
 
Kwahiyo hizo zingine zinatumia line yoyote tu (Huawei, ZTE etc
 
Sio kila router/wifi inaweza kupokea SiM card zengine zinetengenezwa kuungwa na wired network, so hakikisha unanunua yenye uwezo wa SIM, pia zina uwezo tofauti wa kupatana na mitandao tofauti hasa kwenye masuala ya 4G etc so inabidi uhakikishe inapatana na line unayotaka kutumia.

Pia hizi ambazo ni za kampuni za simu mara nyingi ziko locked kwa mtandao mmoja.
 
Asante sana CHIEF MKWAWA
 
Ahsante mkuu, maana Kwa promotion zinazofanywa na mitandao imetufanya wengi kuzoea fikra za Kila mtandao unakuwa na router yake
Jambo jengine muhimu ni kuhakikisha band zinafanana. Tanzania 4G tunatumia
Band 3 (1800mhz) Voda, Airtel, TTCL, Tigo (katikati ya jiji)

Band 7 (2600) Halotel

Band 20 (800) Tigo Nchi nzima na Smile

Band 40 (2300) TTCL.

Kabla kununua router kagua hizo band
 
Shukrani kiongozi
 
Chief-Mkwawa nataka agiza hii router toka ebay,msaada itaweza support band za mitandao ya kwetu hapa. Hasa voda na tigo
 

Attachments

  • Screenshot_20241128_050838_Chrome.jpg
    114.6 KB · Views: 9
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…