Katiba ijayo nipeni nchi na serikali yangu

Katiba ijayo nipeni nchi na serikali yangu

fikirikwanza

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
7,452
Reaction score
3,071
Nikiwa MTZ, ninaomba katiba ijayo irejeshe nchi na serikali mikononi mwa wananchi, katiba iseme wazi namna tunavyoweza mtoa rais kwa kupitia bunge na kupitia wananchi bila kutumia nguvu au vurugu.

Serikali iwe ya wananchi kwa ajili ya wananchi na maslahi ya nchi. Rais ajaye asipewe uwezo wa kuchagua serikali yote yeye pekee yale, RC asiwepo na DC pia. Meya apigiwe kura na wananchi na ndio kiongozi mkuu wa mkoa au mikoa kama majimbo yatapita.

Wakurugenzi wote waombe ajira kupitia kamati maalumu ya wataluma, recruitment commettee for top government autonomous bodies.

Rais akae madarakani miaka 7, na maamuzi ya bunge yawe ya mwisho ktk siasa, kama za ndani ya nchi, ila kama mtu anapenda anaweza kwenda mahakamani na kusikilizwa, haki itolewe mahakamani kama ilivyo sasa.

Baraza la mawaziri lisizidi watu 20, naibu waziri wawe wizara chache tu kama 7-10 basi.

Ungetaka katiba ijayo iweje?? nitafurahi ukiongeza mistari hapa.
 
Back
Top Bottom