Katiba inayopendekezwa imeainisha tunu za taifa

Katiba inayopendekezwa imeainisha tunu za taifa

Dragunov Sniper

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
2,795
Reaction score
9
Tunu ni kitu adhimu, ni kitu cha pekee, ni hidaya, ni zawadi.

Katiba Inayopendekezwa katika Ibara ya 5 imeainisha tunu za Taifa, hivyo tunu hiyo ni kitu ambacho kwa muktadha wa Ibara hii ni zawadi pekee kwa taifa letu. Lakini pia Katiba Inayopendekezwa inazitaja tunu za taifa kwa lengo la kulitanabahisha taifa letu juu ya umuhimu wa kuzienzi na kuzilinda kama mboni ya macho yetu.


Tunu hizi zinazotajwa hapa ni lugha yetu ya Kiswahili, Muungano wetu, utu na udugu, na amani na utulivu kwani tunu hizi zitakuwa muhimili mmojawapo wa kujenga umoja na utangamano wa kitaifa.
 
Back
Top Bottom