Dragunov Sniper
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 2,795
- 9
Mara kadhaa tumesikia kilio cha wananchi wa ngazi zote wakitaka nchi yetu iwe imara na madhubuti katika kuweka na kuzingatia utawala bora.
Katiba Inayopendekezwa katika IBARA YA 6 inaiweka wazi misingi ya utawala bora kama masharti ya kufuatwa na viongozi na watumishi wa umma.
Kuiweka misingi hii katika ibara ya 6 (na siyo ibara ya 5 inayohusu tunu za taifa) ni kuifanya iwe kipimo cha utendaji na utumishi wa umma. Huu utakuwa ni wajibu na si hiyari ya mtumishi wa umma kuamua kama anaienzi misingi hiyo au la, tofauti na kama ambavyo angeweza kuzienzi tunu zilizomo kwenye ibara ya 5, lakini zisingeweza kuchukuliwa kama kigezo cha kupima uwajibikaji na utendaji wake kwa umma endapo atashindwa kuizingatia.