Katiba inayopendekezwa imezingatia maadili ya viongozi na watumishi wa umma

Katiba inayopendekezwa imezingatia maadili ya viongozi na watumishi wa umma

Joined
Mar 7, 2015
Posts
21
Reaction score
1
MAADILI YA VIONGOZI NAWATUMISHI WA UMMA YAMEZINGATIWA NA KUSIMAMIWA VEMA KATIKA KATIBA INAYOPENDEKEZWA.

MAKALA NO. 7


Nachukua fufusa hii kuishukuru Tume ya mabadiliko ya katiba kwa kujali umuhimu wa kuwepo misingi ya maadili ya viongozi wa umma ndani ya katiba kwa maslahi ya watanzania wote. Ningumu sana nchi pamoja na wananchi wake kupata maendeleo ikiwa jamii ya watawala haina misingi mizuri ya maadili ya utumishi wa umma. Katika rasimu ya pili ya katiba iliyopendekezwa suala la maadili kwa viongozi wa umma yalitiliwa mkazo kwa kiasi kikubwa sana na bila shaka maadili ndiyo msingi muhimu wa uwajibikaji kwa viongozi wa umma kwa maslahi ya Taifa.


Ukiukwaji wa maadili ya utumishi wa umma ndicho chanzo cha rushwa, umasikini, uwajibikaji mbovu pamoja na migogoro katika jamii kwa sababu ya jamii kukata tamaa pamoja na kutowaamini viongozi wenye dhamana ya kuwatumikia.


Tangu rasimu hii ilipowasilishwa kwa Mh. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na baadae kuwasilishwa na Mh. Jaji Joseph Sinde Warioba katiba bunge maalum la katiba kumekuwepo na kauli nzito na zalawama dhidi ya bunge maalum kutoka kwa baadhi ya wanasiasa, wale wanaojiita wanaharakati, baadhi ya waliokuwa watumishi wa Tume ya mabadiliko ya katiba pamoja na makundi mbalimali ya kijamii kwamba bunge maalum la katiba halikuzingatia kabisa na hatimae limefuta na kutupilia mbali misingi ya maadili ya viongozi pamoja na watumishi wa umma nakwamba katiba pendekezwa haina misingi hiyo ya maadili hivyo haifai kukubaliwa na wananchi.


Kwa heshima na taadhima kwa watanzania wenzangu, ninaomba niwasihi kuwa watulivu na kuwa na utamaduni binafsi wa kutopenda kuishi kwa kusikiliza yanayosemwa bila kujipa nafasi ya kufuatilia mambo kwa kina. Pia niwasihi watanzania wote wenye uwezo wa kusoma na kuelewa maandiko wawe wanasoma na kuelewa wasipende urahisi wa kusikia tu kutoka kwa watu bila wao kujisomea na kuelewa.

Tabia na utamaduni wakutojisomea na kufuatilia mambo kwa kina nihatari sana na jamii inaweza kupotoshwa hatimae kuishia kulaumu bila sababu za msingi ila tu kwa uvivu wa kutopenda kusoma na kuelewa. Baada ya wanasiasa kugundua kwamba watanzania wengi hatuna utamaduni wa kujisomea ila tunawategemea wao watwambie wameanza kucheza na akili zetu kwa kadri watakavyo na wamefanikiwa kutufikisha hapa tulipo.


Kwa upande wangu nimejitahidi kujitoa kuwafungua macho na fikra watanzania wenzangu ili tupate kuelewa kwa pamoja namna ya mchakato huu wa katiba ulivyokwenda na rasimu ya katiba inayopendekezwa ilivyo kw auhalisia wake.


Ndugu watanzania wenzangu, ninachukua nafasi hii kuwafahamisha kwamba wale wanaosema kwamba misingi ya maadili haikuwekwa katika katiba pendekezwa ni waongo sana, misingi ya maadili kwa vingozi na watumishi wa umma imewekwa na kuzingatiwa katika katiba pendekezwa kama ilivyokuwa katika rasimu ya Tume ya Jaji warioba. Tena bunge maalum kwa kuona umuhimu wa hili katiba pendekezwa ina sura nzima inayohusu maadili na miiko ya ungozi kwa viongozi na watumishi wa umma tena kwa mapana sana katika ibara mbalimabli za katiba pendekezwa.


Sura ya nane ya rasimu ya katiba pendekezwa ndiyo imebeba maudhui ya maadili na miiko ya uongozi na utumishi wa umma ambapo sura ya kwanza inahusu maadili ya uongozi na utumishi wa umma na sehemu ya pili inahusu miiko ya uongozi wa umma.


Ibara ya 28(1) (a) pia ibara ndogo ya (2) inaeleza vema maana ya dhamanaya uongozi wa umma na imeweka wazi kwamba madaraka anayopewa kiongozi wa umma ni dhamana na atatumia madaraka hayo na kutekeleza wajibu wake kwa kuzingatia mashariti ya katiba hii. Kwa hiyo iko wazi kwamba kiongozi wa umma atabanwa na mashariti ya katiba hii na hatoweza kwenda kinyume na matakwa ya katiba hii. Pia misingi mingine mingi na muhimu ya kulinda maadili imewekwa katika ibara hii.


Ibara ya (29) (1) (a-c) inataja na kubainisha kanuni za uongozi wa umma ambapo katika ibara ndogo ya (2) (a-h) bunge limepewa wajibu wa kutunga sheria zitakazosimamia maadili ya viongozi wa umma pia katika ibara ndogo ya (3) katiba imeweka wazi bila kubagua kwamba viongozi wa umma inajumuisha viongozi wa kuteuliwa pamoja nawale wakuchaguliwa. Pamoja na mambo mengine, dhamira pamoja na mazingatio ya kuweka misingi mizuri ya maadili kwa bunge maalum imejidhihirisha wazi katika ibara hii ndogo ya (2) ambapo katiba hii inalielekeza bunge kutunga sheria itakayoanzisha mitaala inayohusu katiba, maadili na uraia, shuleni na vyuoni.

Niwazi kwamba katiba imetengenezwa katika misingi imara ya kuwa na mizizi ya kuondoa tatizo la kukosekana kwa maadili katika nchi yetu kwa kuwa jamii itakuwa inaandaliwa kuanzia chini kujali misingi ya maadili, hakika hii katiba pendekezwa ni nzuri mno na hongereni sana wabunge wote wa bunge maalum mlioshiriki kuitunga katiba hii.


Sehemu ya pili ya sura ya nne ya katiba pendekezwa inahusu miiko ya uongozi wa umma katika ibara za 29 pamoja na 30. Ibara ya 29 (1) inamlazimisha kiongozi wa umma kuheshimu na kutii miiko na maadili ya uongozi wa umma, ibara ndogo ya (2) inatoa wajibu kwa bunge kutunga sheria zitakazoainisha miiko inayotakiwa kuzingatiwa na kiongozi wa umma, kuweka utaratibu wa kumwondoa kazini kiongozi wa umma atakayekiuka miiko na maadili ya uongozi wa umma, kuanisha vitendo ambavyo kiongozi wa umma hatakiwi kuvitenda pia bunge litaainisha orodha ya viongozi wa umma watakaofungwa na ibara hii. Vilevile ibara ya (31) imeweka wazi marufuku vitendo ambavyo kiongozi wa umma hatoruhusiwa kuvitenda.


Ndugu watanzania wenzangu, ninaomba mfahamu kwamba katiba ni sheria mama inayoweka misingi mikuu ya kufuatwa na mihimili ya serikali, viongozi wake pamoja na wananchi wote. Katiba siyo sheria inayotafsiriwa na mahakama katika kutenda wajibu wake. Tumeona ndani ya katiba hii pendekezwa misingi ya maadili imewekwa na pia bunge linapewa wajibu wa kikatiba kutunga sheria za kuitafsiri katiba ili kulinda miiko na kuhakikisha maadili yanakuwepo kwa viongozi na watumishi wa umma.


Katiba imejitoshereza sana katika eneo hili, wajibu uliobaki ni wawabunge watakaokuwa na jukumu la kutunga sheria kuhakikisha wanatunga sheria nzuri na zenye meno makali ya kuwatafuna viongozi na watumishi wa umma watakaokiuka miiko na maadili ya utumishi wa umma. Jambo muhimu la kuzingatia na kushukuru nikwamba kwa mujibu wa katiba hii pendekezwa suala la miiko na maadili ya uongozi kwa watumishi wa umma limekuwa ni la kikatiba kuliko ilivyo sasa ambapo linalegalega kwa kuwa na sheria ambazo hazina msingi mzuri katika katiba tuliyonayo sasa ya (1977)


Katiba inayopendekezwa ina misingi mikali mno ya kuwadhibiti viongozi wa umma iwapo watakiuka maadili kwa mujibu wa katiba hii. Niwazi kwamba kwa muda mrefu kumekuwepo na wizi wafedha za umma kwa baadhi ya viongozi na watumishi wa umma na wamekuwa wakizificha kwenye akaunti za nje ya nchi kutokana na ulegevu wa sheria zilizopo sasa kushindwa kulikabili tatizo hili na hapakuwepo ha hatua za wazi na nzito za kumchukulia kiongozi wa namna hii. Kwa mujibu wa ibara ya 30 ya katiba pendekezwa imelipa wajibu bunge kutunga sheria itakayoweka mashariti kwa kiongozi wa umma kufungua akaunti za nje ambapo niwazi kwamba wizi na ufichaji wa fedha za umma kwenye akaunti za nje kama ilivyo sasa utadhibitiwa.

Pia katika ibara hiyohiyo ya(30) (2) (f) bunge limepewa wajibu wa kutunga sheria itakayoweka utaratibu wa utwaaji wa mali za kiongozi wa umma zinazopatikana kwa kukiuka sheria(maadili na miiko) kama katiba inavyobainisha na sheria itakavyoelekeza.


Ukali kama huu haupo kwenye katiba ya sasa ya (1977) lakini katiba pendekezwa imeweka makali haya kwa viongozi watakaokiuka miiko na maadili ya uongozi na utumishi wa umma. Iko wazi kwamba kwa mujibu wa katiba hii pendekezwa iwapo itapitishwa kwa kura za wananchi historia ya nchi hii itajengeka upya kwa kuwa mwisho wa ufisadi na wizi wa fedha za umma pamoja na uharibifu wa mali za umma.


Katika sura ya 15 katiba inayopendekezwa imetaja Taasisi za uwajibikaji miongoni mwazo ni Tume ya maadili ya viongozi wa umma ambayo imetajwa katika sehemu ya kwanza ya sura hii.

Ibara ya 228(1) inatoa mamlaka ya kikatiba ya kuanzishwa Tume ya maadili ya viongozi wa umma. Ibara ya 229(1) imeweka utarartibu mzuri wa uteuzi wa wajumbe wa Tume hiyo pamoja na sifa zao kwamba wajumbe hao watateuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na kamati ya uteuzi (hapa mamlaka ya Rais ya uteuzi yamepunguzwa) ambapo ibara ya 230 inaainisha muundo wa kamati ya uteuzi ambayo itakuwa na wajumbe huru wanaopatikana kwa mujibu wa katiba na wametajwa nakatiba moja kwa moja.

Kwahiyo wajumbe wa Tume ya maadili ya viongozi wa umma hawateuliwi na Rais moja kwa moja. Pia wajumbe wa kamati ya uteuzi nao hawateuliwi na Rais kufanya kazi yao ila wapo kikatiba na majukumu yao yapo kikatiba hivyo wako huru kufanya kazi zao.


Ibara ya 231(1) inaweka wazi majukumu ya Tume ya maadili na hayana mipaka kwa viongozi wote wa umma kwenye mihimili yote ya dola,taasisi na idara nyingine zote za umma. Tume hii inamamlaka ya kuhakikisha maadili na miiko ya uongozi wa umma inalindwa na kuheshimiwa. Ibara ya 227(1) inatoa uhuru wa Tume ya maadili kufanya kazi bila kuingiliwa na mtu au mamlaka yoyote.


Nadhani wale wanaosema kwamba katiba hii pendekezwa haina maana na kwamba wananchi tusiikubali hawajaisoma na kuielewa au wana ajenda nyingine wanaoijua wao kwa maslahi yao ila kwa kudai kwamba wanapigania maslahi ya wananchi. Katiba hii pendekezwa imeweka misingi mizuri ya kudhibiti miiko na maadili ya viongozi wa umma lakini bado baadhi hawaitaki na ndiyo walikuwa msitari wa mbele kutaka katiba itakayolinda maadili. je, ndiyo kusema kwamba wao hawataki vingozi wa umma wawe na maadili? Au wanaiogopa katiba hii kwa makali yake ndiyo maana wanaikataa?


Kwa mtu yeyote anayetaka Taifa hili lipige hatua ya kimaendeleo na jamii nzima ibadilike kimaisha na kuwa na maisha bora na yenye usawa kamwe hawezi kubeza katiba hii pendekezwa. Tuisome katiba hii kwa kina na tujitokeze kwa wingi kuipitisha katiba hii kwa kura nyingi za ndiyo. TUSIDANGANYIKE TUKIIKATAA TUTAJUTA MWANASHERIA.
MWESIGWA ZAIDI SIRAJI.
0784 646220
 
Back
Top Bottom