MWESIGWA ZAIDI
Member
- Mar 7, 2015
- 21
- 1
KATIBA PENDEKEZWA NIYA KIWANGO CHA JUU NA INAFAA KUPIGIWA KURA NA WANANCHI: misingi muhimu ya kikatiba imezingatiwa.
MAKALA NO. 8
Tunapozungumzia katiba nzuri tunatakiwa kufahamu kwamba lazima iwe imejengwa katika misingi mizuri ya kikatiba ( principles of good constitution). Hii inamaana kwamba katiba ndiyo mwongozo na kanuni kuhusu namna ambavyo madaraka yatapatikana, namna yatakavyotumika, wajibu wa watawala na watawaliwa, haki na wajibu wa watu katika nchi, pamoja na muundo wa vyombo vya uwajibikaji katika nchi.
Hivyo kitaaluma ili katiba ikidhi matakwa yakisheria (Legal Constitutional value) ni lazima iwe imejengwa katika misingi ya kutambua na kulinda haki za binadamu tena kwa usawa yaani haki za makundi yote ya kijamii zilindwe na katiba (principles of Human Rights, majority and minority rights), utaratibu mzuri wa kutunga sheria (Parliamentary legislative procedure), utawala wa sheria, (Rule of Law and due process of Law as well as equality before the Law), mgawanyo mzuri wa madaraka miongoni mwa mihimili ya dola,(Clear Separation of Powers) pamoja na udhibiti wa utendaji wa vyombo vya serikali (Checks and balances), na demokrasia kwa maana ya ushiriki wa wananchi wengi katika masuala ya kitaifa yanayoathiri maisha yao katika Nyanja za siasa, uchumi, utamaduni pamoja na kijamii. (popular participation) (Rejea Philips H.Constitutional and administrative law. 7[SUP]th[/SUP] Ed.1987, Wheare K.C, Moderm Constitutions, oxford university press, London 1964, Wade, ECS&Philips, H.Constitutional law, London, 1965). Misingi mingine midogo inatokana nahii misingi mikubwa na muhimu ya kikatiba.Katiba ya watanzania tunayoitaka lazima iwe inakidhi kwa kuwa nahii misingi mikuu ya kikatiba ili iwe na sifa za kukubalika.
Siyo sahihi kujadili katiba inayopendekezwa kwa kuipima pamoja na rasimu ya Tume. Tunatakiwa kuijadili katiba kwa kuzingatia misingi mikuu ya kikatiba hapo ndipo jamii itaelewa kama katiba inayopendekezwa inawafaa au la. Ikumbukwe kwamba katika historia ya nchi yetu hii nimara ya kwanza kuandika katiba inayotokana na watu wenyewe (popular sovereignty) hivyo lazima tofauti zijitokeze miongoni mwa wadau wa katiba. Lakini itakuwa vizuri tofauti hizi zikijikita katika misingi ya kitaaluma badala ya kubishana tu bila kujenga hoja zinazoweza kuwasaidia watanzania kufahamu maudhui ya katiba pendekezwa.
Kwa bahati mbaya hoja nyingi za kuikataa katiba pendekezwa zimejaa mapenzi na matakwa ya vyama vya siasa zaidi kuliko uhalisia wa kitaaluma pamoja na namna rasimu ya katiba yenyewe namna ilivyo. Ninashawishika kusema kwamba wengi wao hawajaisoma na kuilewa katiba inayopendekezwa au wamekwishaielewa ila hawaitaki tu kwasababu nilizotaja hapo juu. Katiba pendekezwa imejengwa katika misingi sahihi kwa mujibu wa matakwa ya taaluma ya katiba na imezingatia maslahi ya umma kwa kiasi kukubwa.
Katiba hii inatoa dira ya maisha ya watanzania katika Nyanja zote muhimu za maisha. Ibara ya 13 inalenga kujenga uchumi imara kwa watanzania, ibara ya 14 inalenga kujenga jamii imara, ibara ya 15 inalenga kuimarisha utamaduni wa taifa na mtanzania, na ibara ya 12 inalenga kukuza ushiriki wa watanzania katika masuala ya siasa, pia haya yote yamefanywa kuwa malengo ya kitaifa.
Ibara ya 5(a-d) inataja tunu za Taifa kwamba ni lugha ya Kiswahili, muungano,utu na udugu pia amani na utulivu. katiba hii inalenga kuwafanya watanzania wawe wamoja na wenye kuthaminiana. Ibara ya 7 inatambua kwamba wananchi ndiyo msingi wa mamlaka ya nchi hivyo inawapa nguvu wananchi juu ya serikali yao.
Ibara ya 9(1) inaipa katiba hii ukuu kwamba sheria zote za nchi zitatakiwa kulinda misingi ya katiba hii nakwamba katiba hii ndiyo sheria mama. Kutokana na ibara hii iko wazi kwamba hakuna upenyo wa kutungwa wala kutekeleza sheria kandamizi zinazokiuka misingi ya katiba hii.
Ibara ya 17(1) inaitaka serikali kuhakikisha inatengeneza na kusimamia dira ya Taifa ya maendeleo. Hii inamaana kwamba Serikali inao wajibu wa kikatiba kuhakikisha inaweka mipango ya maendeleo kwa manufaa ya watu wake. Kuhusu kuimarisha muungano ambao pia umetajwa kuwa miongoni mwa Tunu za Taifa, ibara ya 18(1) inaitaka serikali kuunda Tume ya mipango ya jamhuri ya muungano.
Ibara ya 25 inaweka jukumu kwa serikali kuhakikisha inalipa fidia stahiki iwapo ardhi ya mwananchi itachukuliwa na serikali kwa shughuli za matumizi ya maendeleo ya umma. Kwa mujibu wa ibara hii mwananchi analindwa kunyonywa na serikali.
Kwa muda mrefu pamekuwepo haja ya kuhakikisha viongozi na watumishi wa umma wanazingatia maadili katika uwajibikali wao na iko wazi kwamba jamii imeathirika kimaendeleo kutokana na wizi wa fedha za umma unaofanywa na baadhi ya viongozi na watumishi wa umma.
Ibara ya 28 inaweka misingi ya ya maadili ya uongozi na utumishi wa umma ambapo kiongozi na mtumishi wa umma atatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia misingi hii. Ibara za 30 na 31 zinataja miiko na kanuni za uongozi wa umma ambapo Tume ya maadili ya viongozi kwa mujibu wa ibara ya 228(1) kutakuwa na Tume ya kusimamia maadili kwa viongozi na watumishi wa umma na inayo meno kikatiba ya kulishighulikia suala la maadili. Kwa hiyo katiba hii imejengwa katika misingi ya kulinda maadili kwa viongozi pamoja na watumishi wote wa umma.
Ibara ya 40(1) (a) na (b) inaweka u huru wa habari pamoja na vyombo vya habari na bunge litatunga sheria kuhakikisha haki hii ya msingi inalindwa kwa mijibu wa sheria. Haki za wafanya kazi pamoja na waajiri zimetajwa na kulindwa kikatiba katika ibara ya 45. Ibara ya 52(1) inatoa haki ya elimu na elimu ya kujitegemea. Kwa mujibu wa ibara hii jamii itanufaika kwa kupata elimu na jukumu hili imepewa serikali kuhakikisha hili linatekelezeka kwa manufaa ya watanzania wote.
Vijana tukiwa nyenzo na rasilimalim muhimu katika jamii haki zetu zimelindwa na nakatiba hii katika ibara ya 54. Katiba inatupatia vijana haki ya kupata furusa za kushiriki kikamilifu katika Nyanja za siasa , uchumi jamii na utamaduni na katika ibara ndogo ya (2)katiba imeanzisha baraz la vijana ambalo bunge litatunga sheria kuhusu namna litakavyofanya kazi kwa maslahi ya vijana. Kwa mujibu wa ibara ya 11,12, 12, 14 na 15 vijana pamoja na maslahi ya vijana yamefanywa kuwa miongoni mwa malengo muhimu ya kitaifa.
Ibara ya 56(1) (a-c) imeweka msingi wa kupatikana haki za makundi madogo katika jamii pia maslahi ya makundi hayo yamelindwa na kuthaminiwa ambayo ni kupata kazi, kupata maeneo ya kuishi, kupewa elimu, kujiendeleza kiuchumi pamoja na kupata ajira. Katiba pia imetambua na kuweka haki za watu wenye ulemavu sawa nawatu wengine katika ibara ya 55 ya katiba pendekezwa. Ibara ya 57(e)imeweka haki na msingi wa kulinda ajira ya mama mjamzito pia ibara hii imetambua na kulinda haki za wanawake. Ibara ya 58 inalinda haki za wazee na kuweka msingi imara wa kuondoa adha kwa wazee kwa kuboresha usalama pamoja na maisha yao, jukumu ambalo ni la serikali.
Kwa muda mrefu kumekuwepo na malalamiko ya kuibiwa na kudhulumiwa wasanii kutokana na kutokuwepo msingi wa kikatiba wa kulinda haki zao. Kutokana na uhalisia kwamba vijana wengi wanazidi kuwa wabunifu na kujiajiri kupitia kazi za sanaa, katiba pendekezwa katika ibara ya 59 imeweka haki ya uhuru wa taaluma, ubunifu, ugunduzi na usanii nahaki za kundi hili zimelindwa kikatiba.
Miongoni mwa malengo makuu ya kitaifa nipamoja na lengo la kiuchumi katika ibara ya 13, ibara ya 61(1) inaweka wajibu wa kushiriki kazi ili kufikia lengo hili muhimu ambapo lengo hili linaenda sambamba na matakwa ya ibara ya 54(1) ambayo inatoa haki kwa vijana kupatiwa furusa za kushiriki kikamilifu katika Nyanja za siasa, uchumi, jamii na utamaduni.
Kuhusu Rais kukiuka katiba, ibara ya 97(1) inalipa bunge mamlaka ya kumshitaki na kumuondoa Rais madarakani iwapo atatenda vitenda vya ukiukwaji wa katiba kwahiyo Rais hayuko salama na hana ulinzi iwapo atakiuka katiba ya nchi. Ili kuhakikisha maendeleo yanapatikana katika kwa wananchi, ibara ya 124 (1) imeanzisha serikali za mitaa na ibara ya 125 serikali hizo zinawajibu wakikatiba kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo kwenye maeneo yao, pia umma umekuwa na nafasi pana kushiriki katika serikali yao kwa kugatua madaraka kwa wananchi ili kukuza ushiriki wa wananchi katika mambo ya maendeleo.
Ibara ya 127(1) imeanzisha Tume ya usimamizi na uratibu wa mambo ya muungano kwa lengo la kuhakikisha utekelezaji wa mambo ya muungano unafanikiwa kwa manufaa ya wananchi wa jamhuri ya muungano pamoja na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.
Bunge nalo halikuachwa huru kama ilivyo kwa sasa. Kwa kutambua kwamba wabunge watatokana na wananchi wanawajibika kuwatumikia wananchi pia kuhakikisha utumishi wao katika bunge unakuwa na tija kwa taifa. Ibara ya 155 imeanzisha Tume ya utumishi wa bunge na ibara ya 160 (1) na ibaraya 161 inaipa jukumu Tume hiyo ya kulisimamia bunge ili kufanya kazi kwa ufanisi.
Ili kuongeza wigo wa upatikanaji wa haki za kisheria, katiba pendekezwa imeanzisha mahakama ya juu(supreme court) katika ibara ya 171 ambayo miongoni mwa mamlaka yake itakuwa nipamoja na kusikiliza rufaa zitakazotoka mahakama ya rufaa. Hii imeongeza wigo wa kupatikana haki tofauti na silivyo sasa mahakama ya rufaa ndiyo ya mwisho kimaamuzi. Pia itakuwa na jukumu la kuzishauri serikali zote mbili, kusikiliza mashauri yanayohusu matokeo ya Rais na kutoa ushauri kuhusu mambo ya muungano.
Mahakama kama chombo huru cha kutafsiri sheria na kusimamia haki, ibara ya 204(1) imeweka Tume ya utumishi wa mahakama ili kuhakikisha watumishi wa kada hii wanatekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria bila kuvunja mashariti ya katiba ya nchi. Ibara ya 210 inahusu uwepo wa Tume ya utumishi wa umma ambapo Tume hii itakuwa na jukumu la kushughulikia nidhamu na mambo yote ya utumishi pamoja na kuhakikisha haki za watumishi zinasimamiwa vema.
Ili kuhakikisha maslahi ya watumishi yanalindwa na kusimamiwa vema kwa mujibu wa katiba hii, katiba pendekezwa katika ibara ya 213(1) inaipa wajibu serikali wa kuwepo Tume ya mishahara ambayo itashughulikia mishahara pamoja na maslahi mengine ya watumishi, hii pia nidhamira ya serikali kujali maslahi ya watumishi wote.
Lengo la Taifa kisiasa la kukuza dsemocrasia lililoainishwa katika ibara ya 12 linajidhihirisha katika ibara ya 216(1) ambapo mgombea huru anatambuliwa katika katiba hii na anahaki sawa za kisiasa kama ilivyo kwa wagombea wengine kutoka vyama vya siasa. Ibara ya 217(1) inatambua uwepo wa Tume huru ya uchaguzi ambayo wajumbe wake hawateuliwi na Rais moja kwamoja kama ilivyo kwa sasa na badala yake wanapendekezwa na Kamati ya uteuzi na majina stahiki kupelekwa kwa Rais ili kuteua wajumbe wa Tume ya uchaguzi.
Ili kuhakkisha kuwepo kwa utawala bora ibara ya 249 imeanzisha chombo cha kuzuia na kupambana na rushwa. Pia ibara ya 243 imeweka ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ili kuhakikisha fedha za umma zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa. Katiba pendekezwa katika ibara ya 6(2) (a-j) imeweka misingi ya utawala bora kuwa ni: uadilifu, democrasia, uwajibikaji, utawala wa sheria, ushirikishwaji wa wananchi, haki za binadamu, usawa wa jinsia, umoja wa kitaifa, uwazi na uzalendo. Haina shaka kwamba kwa katiba hii watumishi wa umma watawajibika kwa maslahi ya wananchi pamoja na Taifa.
Kwa kuzingatia uhai wa watanzania, katiba pendekezwa katika ibara ya 51 imeweka haki ya maji safi na salama, hii inamaana kwamba suala la kupatikana maji safi na salama niwajibu wa serikali kikatiba kuhakikisha yanapatikana. Kwa kuzingatia kwamba wakulima, wafugaji, wavuvi pamoja na wachimbaji madini ni kundi kubwa sana na muhimu kwa maendeleo ya Taifa, katiba pendekezwa katika ibara ya 46 imetambua na kulinda haki za makundi haya muhimu sana katika jamii. Haki za makundi haya zinalindwa na sheria mama ya nchi ambayo ni katiba.
Kwa muda mrefu pamekuwepo na kilio cha kisiasa kuhusu kutokuwepo haki ya kikatiba ya kupinga matokeo ya urais iwapo kuna sababu za kufanya hivyo, hata mimi ninaungana na wale waliokuwa nakilio hiki kwa kuwa democrasia ilikuwa imekanyagwa katika katiba tuliyonayo sasa ya (1977). Ibara ya 90 ya katiba pendekezwa inatoa haki kwa mgombea ambaye hatoridhika na matokeo ya urais kupinga matokeo hayo kwenye mahakama ya juu ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kusikiliza shauri lka namna hii. Kwa mujibu wa ibara hii tunaona wazi kwamba nikweli lile lengo lakatiba hii la kitaifa la kukuza demokrasia na ushiriki mpana wa kisiasa katika ibara ya 12 linajidhihirisha kwa ibara ya 90 kutoa haki ya kupinga matokeo ya urais kwa mgombea ambaye hatoridhika na matokeo yatakayotangazwa na Tume ya uchaguzi ya Taifa.
Ili kuhakikisha jamii inapata huduma stahiki katiba pendekezwa katika ibara katika ibara ya 214 inalipa bunge wajibu wa kutunga sheria itakayoanzisha Tume mbalimbali za kisekta kwa ajili ya usimamizi, uratibu na utoaji wa huduma za jamii. Kwa mujibu wa ibara hii, wizara, idara pamoja na Taaasisi zote za umma zitakuwa zikiangaliwa namna ya utendaji wake wa kazi kwa manufaa ya watanzania.
Kutokana na uzuri na ubora wa katiba hii pendekezwa kukidhi matakwa ya kikatiba (Constitution Value) hata ningepata wino sawa na ujazo wa maji ya bahari, wino huo utaisha bila kumaliza kueleza ubora wa katiba hii. Haipendezi kwa mtu au watu wenye uwezo wa kusoma na kuelewa wakawa ndiyo tatizo la kusambaza uongo kwamba katiba hii haina ubora na kwamba haina tofauti na katiba ya 1977 tunayotumia sasa wakati katiba pendekezwa inautofauti mkubwa sana ukilinganisha na katiba ya 1977 na imejali sana maslahi ya watanzaniakatika Nyanja zote za kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kijamii MWANASHERIA.
MWESIGWA ZAIDI SIRAJI. (0784 646220)