MWESIGWA ZAIDI
Member
- Mar 7, 2015
- 21
- 1
KATIBA INAYOPENDEKEZWA INA UHALALI WA KUPIGIWA KURA NA WANANCHI: HOJA ZA UKAWA ZIPUUZWE, ZINALENGA KUVURUGA AMANI YA NCHI.
MAKALA NO. 4
Kumekuwepo na kauli nzito kutoka kwa baadhi ya vyama vya siasa na hasa kwa wale wanaojiita UKAWA kuhamasisha wananchi kwamba wananchi tusijitoke kuipigia kura ima ya hapana au ya ndiyo katiba pendekezwa kwa madai kwamba Katiba hii haina uhalali na pia ilichakachuliwa na maoni mengi yaliyomo kwenye rasimu ya Tume yameachwa na bunge maalumu la katiba.Msingi mkuu wa hoja yao umejikita kwenye tafsiri ya kifungu cha 25(1) cha sheria ya mabadiliko ya katiba sura ya 83 toleo la mwaka 2014 kuhusu mamlaka ya bunge maalum la katiba kwamba halikuwa na mamlaka ya kubadili, kuongeza hata kurekebisha maoni yaliyokuwemo kwenye rasimu ya tume ya Jaji warioba. Kwamba kitendo cha bunge maalum la katiba kufanya marekebisho katika katiba inayopendekezwa haikuwa sahihi hivyo katiba inakosa uhalali wa kupigiwa kura na wananchi.
Tafsiri pamoja na maoni ya namna hii siyo yakweli kabisa na hayazingatii mantiki ya kisheria ya kifungu hiki. Tafsiri nyingi kuhusiana na jambo hili zimejikita kwenye maslahi ya kisiasa zaidi kuliko uhalisia wa matakwa halisi ya kifungu hiki cha sheria ya mabadiliko ya katiba pamoja na dhana halisi yakisheria naya kisiasa kuhusu bunge maalum la katiba.
Binafsi ninasema kwamba Bunge maalum la katiba kazi liliyofanya ya kubadili, kurekebisha na kuongeza baadhi ya mambo muhimu nihalali kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba na kwa kifungu hicho hicho cha 25 (1) ndicho kinalipa bunge maalum mamlaka ya kufanya hivyo kwa sababu zifuatazo.
Kwanza, bunge maalum la katiba ndicho chombo pekee kilichopewa mamlaka ya kutunga katiba inayopendekezwa kwa wananchi nahii nikwa mujibu wa kifungu cha 28(1) cha sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2014 baada ya tume kukusanya maoni kisha kulipa bunge rasimu kwa ajili ya kutunga katiba inayopendekezwa, hivyo tume ilikuwa nakazi yakukusanya maoni nasiyo kutunga katiba inayopendekezwa. Kazi ya kutunga katiba ilikuwa niya bunge maalum la katiba.
Pili, Yapo mambo muhimu na moani ya wananchi yaliyoachwa na tume na ilikuwa nikazi ya bunge maalum la katiba kuyafahamu na kisha kufanya marekebisho kwa namna ambavyo bunge maalum liliona inafaa nahii nikwa mujibu wa sheria hiyo ya mabadiliko ya katiba fungu la 25(1). Tafsiri ya neno kama litakavyoona inafaa ni discretion yaani hapa bunge lilipewa mamlaka yakipekee na sheria ya mabadiliko ya katiba kuwa na uhuru wake wakufanya mabadiliko katika maoni yaliyowasilishwa na tume ya mabadiliko ya katiba, bunge halikufungwa na rasimu ya Tume kama ambavyo Tume haikufungwa na sheria ya mabadiliko ya katiba katika fungu la 10 la sheria hiyo. kwahiyo kilichotakiwa hapa kwa wabunge wote ilikuwa ni nguvu ya hoja kuwasilishwa na pande husika kwa yale yaliyokuwemo ndani ya rasimu pamoja na yale yaliyokuwa yameachwa na tume ili yakubalike au yakataliwe na wabunge wa bunge maalum la katiba.
Vilevile ifahamike kwamba hii sheria ilitungwa na wabunge wote wa bunge la jamhuri ya muungano ambapo hata hawa wanaoipinga kwasasa walishiriki kuitunga na kuipitisha. Pia kifungu cha 28(1) cha sheria ya mabadiliko ya katiba sura ya 83 toleo la mwaka 2014 kinatoa mamlaka kwa bunge maalum la katiba kutunga katiba inayopendekezwa, hivyo jukumu la bunge maalum la katiba linapatikana kwa kutafsiri kwa pamoja kifungu cha 25(1) na 28(1) cha sheria ya mabadiliko ya katiba. Bunge maalum la katiba halikuwa na kazi ya kupitisha rasimu ya Tume kama inavotafsiriwa na baadhi ya watu, bali lilikuwa pia na mamlaka ya kujadili, kuboresha, kupitisha, kubadili pia kutunga katiba inayopendekezwa ilimradi katika kutunga katiba pendekezwa bunge halitakiwi kutoka kabisa nje ya misingi ya rasimu ya Tume ambayo msingi wake ni wananchi na hivi ndivyo bunge maalum lilivyofanya.
Tatu, Sheria ya mabadiliko ya katiba haikutoa mwanya tena kuwepo tume ya mabadiliko ya katiba kukusanya maoni tena au kufanya marekebisho iwapo mapungufu kama hayo yangejitokeza kama ilivyobainika mara tu baada ya kuwasilishwa rasimu ile kwa bunge maalumu la katiba na badala yake mamlaka ya kurekebisha yalipewa kwa bunge maalum la katiba. Hapa kuna maswali tujiulize. 1.Bunge lingeipitisha rasimu ile ikiwa na mapungufu? 2. Je, ingeundwa tume nyingine wakati sheria hairuhusu?Bila shaka Sheria iliyaona hayo yote ndiyo maana bunge maalum la katiba likapewa mamlaka ya upekee (discretion) ya kuboresha maoni yaliyowasilishwa na tume ya mabadiliko yakatiba.
Pia ikumbukwe na ifahamike kwamba bunge maalum la katiba halikuwa na mamlaka dhidi ya tume ya kuirudishia rasimu ili ifanyiwe marekebisho kwa mapungufu yaliyokuwemo. Je, jukumu la kurekebisha hayo mapungufulilikuwa la nani?
Nne, hoja yakwamba maoni yaliyokuwemo kwenye rasimu ya tume yalichakachuliwa haifafanui nikwa vipi uchakachuaji huo ulifanyika ila ni kauli tu zakisiasa zisizothibitika na haziwezi kuthibitika kisheria wala kimazingira. Pia ifahamike kwamba kanuni zilizoliongoza bunge maalum zilitengenezwa na kupitishwa na bunge maalum la katiba, kanuni ambazo zilipelekea kupatikana kwa katiba inayopendekezwa.
Kama hoja nikurekebishwa serikali tatu na kuwa mbili pia nayo nimamlaka ya bunge maalum kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko yakatiba fungu la 25 (1) na 28(1) ya sheria ya mabadiliko ya katiba kwa kuwa hata mapendekezo ya muundo wa serikali mbili pia yalikuwemo kwenye rasimu ya Tume, pia wapo wananchi waliopendekeza muundo wa serikali mbili, siyo jambo lililozushwa na bunge maalum la katiba. kwa hiyo bunge maalum kupendekeza muundo wa serikali mbili pia ni sahihi kwa sababu msingi wake ulitoka kwenye rasimu ya Tume, hata hivyo muundo wa serikali tatu uliopendekezwa na Tume haukuwa imara kuweza kudumu kutokana na Tume kushindwa kutengeneza mfumo mzuri wa kiuchumi na kiutawala wakuulinda muungano wa shirikisho wa serikali tatu uliopendekezwa na Tume.
Vilevile ikumbukwe kwamba katiba inayopendekezwa kwa kiasi kikubwa imetokana na rasimu ya Tume na ilipitishwa kwa wingi wa theluthi tatu ya wajumbe wa bunge maalum la katiba kutoka sehemu zote mbili za muungano kama sheria ya mabadiliko ya katiba toleo la mwaka 2014 inavyotaka.
Hivyo kwa maoni na ufahamu wangu ambao nina amini ni sahihi kisheria na kiuhalisia, bunge maalum lakatiba limeleta katiba inayopendekezwa ambayo ni halali kwa kuwa hakuna sheria wala utaratibu wa matakwa ya sheria ya mabadiliko ya katiba uliovunjwa au kukiukwa na bunge maalum la katiba katika mchakato mzima wa kuipata katiba inayopendekezwa.
Pia hoja yao ya kutoshiriki mchakato wa kura ya maoni ni sahihi kwao kama vyama vya siasa ila wasitushawishi sisi wananchi kutoshiriki kwa kuwa hawalazimishwi kushiriki katika mchakato huu wao kama chama Fulani isipokuwa sheria iliingiza vyama vya siasa kushiriki mchakato wa katiba kutokana na umuhimu wao wa uwakilishi wa wananchi ila siyo makusudio ya sheria kuvipa vyama nguvu ya kuhodhi mchakato wa katiba, Walengwa wakuu wamchakato huu nisisi wananchi, mchakato niwetu wananchi hivyo kutoshiriki kwenu kama vyama vya siasa ni matakwa yenu yakisiasa nasiyo kwa maslahi yetu wananchi kama vyama hivyo mnavyojinadi. Bila shaka sisi wananchi ndiyo tutawahukumu kwa kuwa mlituomba dhamana ya madaraka kwa ahadi ya kututumikia ila kwa sasa mmetugeuka na kuanza kusimamia maslahi yenu na siyo yakwetu kama mlivyotuahidi kipindi mnatuomba kura zetu. je, kututumikia ndiyo kususa na kutoshiriki mchakato wa kura ya maoni?
Je, kutoshiriki kwenu kutaondoa uhalali wa katiba iwapo itapitishwa na wananchi waliowengi? Je, iwapo katiba inayopendekezwa itapitishwa kwa wingi wa kura za wananchi ninyi mnaoikataa mtashiriki mchakato wa siasa kwa katiba ipi? ninyi mnaosusa kushiriki mchakato wa kupatikana katiba mpya mmekomaa kisiasa? Katiba mpya siyo ya vyama vya siasa hivyo kususa kushiriki michakato muhimu yakutuletea maendeleo wananchi wa Tanzania nikutusaliti na kutotimiza wajibu wenu wa kutuwakilisha kisiasa. Kilichobaki nisisi wananchi kutafakari kwa kina kama kweli hiyo ndiyo njia sahihi ya kutupatia masilahi yetu kama wanavyosema na kama siyo, nini chakufanya ili maslahi yetu yawasilishwe na kutetewa vyema kisiasa.
Kuhusu hoja hii ya kutoshiriki mchakato wa kura ya maoni inayotolewa na baadhi ya vyama vya siasa ninawasahauri yafuatayo Vyama vyote vishiriki mchakato na kutuelimisha mazuri au mapungufu wanayoyaona katika katiba inayopendekezwa ili tuwaelewe na hatimae tuamue kwa kuipigia kura katiba pendekezwa kama tutakavyoona inafaa ili lengo lao la uwakilishi kisiasa likamilike. Pia wafahamu kwamba kuendelea kususa kutuwakilisha katika mambo muhimu yanayoathiri maisha yetu tutawachoka na tutawapa kichapo kikali cha kisiasa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu
Pia kususa michakato muhimu ya kisiasa halitokuwa jambo jipya kwa kuwa tayari mlisusa mchakato na iwapo mtashiriki nisawa na kutwambia sisi wananchi kwamba kipindi mliposusa hamkuwa na sababu za msingi nasasa mmeona sababu za msingi za kushiriki mchakato ambazo hapo mwanzoni hamkuziona au mliziona ila mlikaidi tu bila sababu za msingi. Au mtwambie kwamba nguvu zenu, uwezo wenu pamoja na ushawishi wenu kisiasa ulikwisha kuanzia bungeni hadi sasa mmejipima na kuona kwamba nguvu yenu ya ushawishi wa kisiasa ni ndogo mno na hivyo kuamua kususa. Kwa niaba ya watanzania, ninyi mnaosusa mchakato huu ninaomba mtuelimishe sababu muhimu za kususa na kuendelea kutushawishi tususie mchakato huu muhimu kwetu.
Kwa muda tunaoendelea kuwasubiria mtuelimishe, kutokana na sababu nilizotoa hapo juu ambazo ninaziona na kuziamini kwamba mchakato wakupatikana katiba mpya haukukiuka sheria wala utaratibu wowote, ninawashauri watanzania wenzangu tushiriki mchakato wa kura yamaoni kuanzia kujiandikisha na tuipigie kura ya ndiyo katiba pendekezwa kwa kuwa imezingatia masilahi yetu ya kiucumi, kisiasa, kijamii na kiutamadaduni kwa kina.
MWANASHERIA MWESIGWA ZAIDI SIRAJI 0784 646220