Katiba Inayopendekezwa inatambua haki za vijana.

Katiba Inayopendekezwa inatambua haki za vijana.

Dragunov Sniper

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
2,795
Reaction score
9
IBARA YA 54 YA KATIBA INAYOPENDEKEZWA:


Ibara hii ni mpya na ni mara ya kwanza kuwekwa
kikatiba.


Katiba Inayopendekezwa inatambua haki
za vijana na wajibu walionao kwa jamii.


Katiba Inayopendekezwa inaielekeza Serikali kuhakikisha
kwamba vijana wanawekewa mazingira mazuri ya kuwa raia wema na kupatiwa fursa za kushiriki kikamilifu katika masuala ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.


Sambamba na hilo, Katiba Inayopendekezwa inaielekeza Serikali kuanzisha Baraza la Vijana la Taifa. Baraza hili litakuwa muhimu sana kwa vijana kutoka katika makundi mbalimbali ya jamii kupata jukwaa la kupaza sauti zao, kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili na
kushirikiana na Serikali katika kuzikabili.



Sasa hakikisha unaisoma vema Katiba hiyo na uielewe, utajikuta unagundua mambo mengi muhimu ambayo yatakusaidia wewe na jirani yako.
 
Back
Top Bottom