Dragunov Sniper
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 2,795
- 9
Kwa mara ya kwanza katika taifa letu, Katiba Inayopendekezwa katika IBARA YA 46 imeyatambua makundi madogo madogo ya wakulima na wafugaji, wavuvi na wachimba madini ambayo mara kwa mara yamekuwa yakiathiriwa na migogoro ya ardhi.
Kimsingi, makundi yote hayo yana maslahi yanayofanana na kushabihiana kwa kiasi kikubwa. Kutokana na hali hii migogoro imekuwa ikizuka mara kwa mara kwa sababu tu ya kugombania maslahi hayo. Katiba Inayopendekezwa kwa kutambua na kuzingatia ukweli huo, inazitaja na kuzitambua haki za makundi hayo kwa lengo la kuhakikisha kwamba maslahi yao yanalindwa.