Katiba inayopendekezwa ndiyo suluhisho ya yote.

Katiba inayopendekezwa ndiyo suluhisho ya yote.

Dragunov Sniper

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
2,795
Reaction score
9
IBARA YA 23-27 Katiba Inayopendekezwa inataja wazi kuwa ardhi ndiyo rasilimali kuu kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi, kijamii na ustawi wa nchi pamoja na watu wake.

Serikali zetu hizi mbili (SMT na SMZ) zitaweka mipango bora ya matumizi endelevu ya ardhi kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Ili kuhakikisha kuwa ardhi inawanufaisha wananchi, suala la haki ya kumiliki ardhi inatajwa kuwa ni kwa raia wa Tanzania pekee, na mtu ambaye siyo raia wa Tanzania atakuwa na haki ya kutumia ardhi hiyo kwa uwekezaji na maendeleo mengine ya kiuchumi na makaazi.

Lakini ni vema ikafahamika kwamba, suala la haki ya kumiliki ardhi na mali nyingine ni la wananchi wote na vile vile kwa kuona kuwa wanawake wengi katika baadhi ya jamii zetu wamekosa kuifaidihaki hii kikamilifu, ndipo Katiba Inayopendekezwa imeona umuhimu mkubwa wa kuwawekea wanawake ulinzi wa kikatiba katika eneo hili, hivyo kwa mujibu wa IBARA YA 23(2)(d) mwanamke atakuwa na haki sawa na mwanaume ya kupata, kumiliki, kutumia, kuendeleza na kusimamia ardhi. Hii ni kwa mara ya kwanza haki hii inatajwa kwa ufasaha wa aina yake!!
 
Ili kuhakikisha kuwa ardhi inawanufaisha wananchi, suala la haki ya kumiliki ardhi inatajwa kuwa ni kwa raia wa Tanzania pekee, na mtu ambaye siyo raia wa Tanzania atakuwa na haki ya kutumia ardhi hiyo kwa uwekezaji na maendeleo mengine ya kiuchumi na makaazi.

HII NIMEIPENDA SANA!
 
So what??? Unaangalia line mbili katika kitaby chenye kurasa 100 na unasema kitabu kizuri?
 
Back
Top Bottom