gwamaka aswile
Senior Member
- Mar 26, 2015
- 186
- 106
Awali ya yote napenda kuwatoa wasiwasi Watanzania wenzangu ambao kwa namna moja au nyingine wamekuwa na wasiwasi kama Katiba Inayopendekezwa itapigiwa kura ya maoni na kama uchaguzi mkuu utafanyika.
Napenda kuwaambia kwamba Katiba Inayopendekezwa itapigiwa kura ya maoni na uchaguzi mkuu utafinyika kama ilivyopangwa licha ya kasoro chache zilizojitokeza.
Nimeamua kuwatoa wasiwasi Watanzania wenzangu kwa sababu wapo baadhi ya watu wamekuwa wakipiga propoganda kwamba mambo hayo hayatafanyika mwaka huu na Rais Jakaya Kikwete ataendelea kuongoza lengo likiwa ni kukiwekea mazingira mazuri Chama cha Mapinduzi kuendelea kushika madaraka.
Wapo wanaodai kitendo cha kuahirishwa zoezi la kuipigia kura ya maoni Katiba Inayopendekezwa ni moja ya mkakati huo pamoja na kutoichapisha kwa wingi katiba hiyo ili isomwe na kila Mtanzania mwenye sifa ya kupiga kura ili ieleweke.
Napenda kusema, watu hao wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani hawaitakii mema nchi yetu na lengo lao ni kutaka kuleta machafuko.
Ninavyoelewa ni kwamba serikali inafanya mambo yake kwa weledi mkubwa hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi kwani kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa.
:wink2: