PakiJinja
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 11,689
- 25,848
Watawala wanazunguka sana, wanahangaika sana. Kwa muda mrefu Katiba yetu imekua ikitoa kinga kwa rais aliyemaliza muda wake kuja kushitakiwa kwa makosa aliyoyafanya alipokua madarakani.
Kinga imekua ikipigiwa keleke sana, ilifikia mahala tukaona kabisa walebwaliojiita Wazalendo na wenye uchungu na nchi hii wanaenda kuifuta hii sheria, kwani wao hawaihitaji hii sheria kwa jinsi walivyo wazalendo. Cha ajabu watu hawa, badala ya kuifuta, waonwakaongeza idadi ya watu wanaotakiwa kukingwa.
Hali ikaendelea, na sasa hivi, wanaotakiwa kukingwa ni wanausalama wanaotumwa na watawala wataenda kulindwa.
Ushauri wangu ni huu. Pelekeni tu mswada bungeni, mumpe rais na mahakama mamlaka ya kumfukuza Mtanzania yeyote nchini. Hili wala haliwezi kuwa jambo geni, kwani tayari mkuu wa wilaya ana uwezo wa kumfukuza mtanzania yeyote yule wilayani kwake, Mkuu wa mkoa poa ana mamlaka ya kumfukuza mtanzania yeyote yule Mkoani mwake.
Rais, Mahakama na Bunge viongezewe guvu hii, wawe na uwezo wa kufukuza mtanzania yeyote nchini iwapo wataona mtu huyo ni hatari kwa maslahi na ustawi wao.
Wasitumie nguvu nyingi kujilinda, wala kuua, wala kuwabambikia makosa, wajipatie tu mamlaka ya kuwafukuza nchini na atakayegoma kuondoka ndiyonapelekwe jela na kazi ngumu.