sixgates
JF-Expert Member
- Mar 19, 2011
- 3,979
- 1,665
Mchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Dr Benson Banna ambaye kwa mara nyingi uchambuzi wake umekuwa ukitiliwa shaka haswa kwa kuonekana kuegemea CCM na kuitetea serikali kwa kila jambo, leo kupitia kipindi cha Nipashe cha redio one asubuhi hii ameilaani CCM kwa yanayoendelea bungeni kwa kusema ndio kikundi pekee ambacho kinaonekana kimejipanga kukwamisha zoezi la kupata katiba mpya.
" CCM ni chama tawala, unapokuwa kiongozi inabidi uonyeshe mfano, lakini ukiangalia yanayoendelea ni wazi ccm ndio wanavuruga mchakato wa kupata katiba, hata kuandaa mwenyekiti sio kitu kilichopaswa kufanywa na ccm. Ukiangalia utaona ccm wanapinga hata mambo yasiyo na maana, kitu kinachotia shaka sana." Alisema Banna.
Banna akiongea kwa masikitiko, amelaani yanayofanywa na ccm, na kusema wana agenda yao ya siri lazima waache ukweli uprevail.