Katiba Mpya: CCM tumejitengenezea mazingira magumu ya kisiasa

Katiba Mpya: CCM tumejitengenezea mazingira magumu ya kisiasa

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,207
Reaction score
13,839
Mchakato wa kutengeneza katiba mpya ndo umeanza, na mambo yana badilika kila uchao.

Katika mchakato huu wa kihisoria, pengine muasisi wa mchakato huu, Rais Jakaya Kikwete hatasahaulika na wanahistoria watakuwa na maoni tofauti katika hili.

Hata hivyo mchakato mzima unaelekea kukiumbua kwa kiasi fulani Cha cha Mapinduzi, kwa vile hakionekani kama kilikuwa kimejiandaa vyema.

Kuna mambo kadhaa yanayoonyesha kuwa kujiandaa kwa CCM katika mchakato huu yatakiletea msimamo hasi mbele ya jamii.
Naweza kuwa nimekosea katika uchambuzi huu, lakini yanayooneka kisiasa yanaashiria udhhiri wa kukosa msimamo dhabiti katika hili.

La kwanza ni kwamba suala la mchakato wa katiba mpya halikuwa katika ilani ya uchaguzi mwaka 2010.
Mchakato huu umekuja kwa shinikizo toka nje ya chama, hivyo basi wanachama wa CCM hawakuweza kupata muda wakujitayarisha kisaikolojia na kwa kupata mifumo endelevu kwa nchi na chama chao.
Hili halina ubishi.

Pili,Chama hakutoa maoni yakekiufasaha juu ya suala la muungano hasa pale Zanzibar kupitia Baraza la Wawakilishi lilipoamua kujifanyia marekebisho ya katiba Ya Zanzibar bila kutilia maanani nafasi yao na madhara yake kwa muungano.
Kimsingi mabadiliko ya katiba ya Zanzibar ni kama ya repudiate uhalali wa mungano kwa vile Zanzibar waliamua kuwa Nchi.
hatujasahau wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walivyo mdharau mh Miz engo Pinda juu ya hili Bungeni alipolielezea hili kisheria, tukijua kwa ni mwanasheria.

Tatu, ulipoanzishwa mchakato wenyewe kwa kupitia Tume ya Warioba, chama kimejisahau kuwa Tume hii iliwauliza wananchi juu ya kile wakitakacho katika marekebisho ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tume haikuja na mawazo yake yenyewe bali yale wananchi walivyotaka.

Dalili ya kwanza ya kuonyesha kuwa chama sasakimechanganyikiwa ni kilipo anza kumshambulia Mzee Warioba kwa kuonyesha kile wananchi wakitakacho.

Ni kama vile chama kilikuwa kinajaribu kukivunja kioo kinachoonyesha taswira ya kile kinachoonekana ndani ya kioo.
Habari ambazo hazijathibitishwa ni kwamba chama kimetayarisha msimamo wake tayari juu ya kile ikitakacho, maoni ambayo hayana baraka ya wananchi walio wengi.

Hapa ndio nasema chama kinajiwekea mzingira nagumu kisiasa, maana kuna uwezekano mkubwa sana si kupingwa na wananchi tu, bali hata na wanachama wenyewe na dhamira zao.

Kama chama kingependa kurudisha its moral authority, lazima kifanye maamuzi magumu sana.
Kwanza, kuryudisha imani ya wananchi na wanachama kwa kurekebisha kasoro za katiba iliyorekebishwa ya Zanzibar, ili supremacy ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania isitiliwe shaka na mtu yeyote.
Pili chama kione uwezekano wa kuwa na serikali moja tu, ili kuondoa shaka toka pande zote za muungano juu ya dhamira zisizoeleweka.
Tatu, all along chama kimekuwa defensive katika mchakato mzima wa katiba mpya, chama kikae chini kijiulize kilipo jikwaa, maana sana sana inavyoonekana sasa ni kama chama kinalazimisha kutetea nafasi ya viongozi wake bila kufikiria au kuwa pamoja na wananchi.

Mpaka naandika haya, huwa najiuliza wale strtegic thinkers wa chama waliishia wapi?
Lakini kimsingi, hapa tulipo hatukufika kwa bahati mbaya, tumejiwekea mazingira magumu sisi wenyewe.
 
CCM wamejisahau mno , eti leo mshauri wao mkuu kwenye suala la Katiba ni Evod Mmanda.......what a shame.......
 
Wanataka wasaliti wa CCM wajulikane kwa kuweka kura ya wazi kwenye kupitisha katiba, eti CCM leo ndo wanapigania uwazi kwenye maamuzi? wakati mikataba ni siri, kila kitu kwenye utawala wao ni top secret kuna nini leo wanataka uwazi kwenye kupitisha katiba.. Anywa either ways iwe kura ya siri au ya wazi it will all backfire on CCM..
 
Kwenye maandiko kuna neno lisemalo "aonywaye mara nyingi akishupaza shingo yake atavunjika ghafula". Suala la Katiba kama mfumo wa vyama vingi haikuwa agenda ya ccm...hii imelazimishwa na kinachoitwa "nguvu ya umma". Matokeo ya kulazimishwa wakati wao hawako tayari ni utumiaji mkubwa wa mabavu kuhalalisha uwepo wao kwenye kushika dola, kutokutaka kusikiliza waliowaweka madarakani (wananchi) wanasemaje na kiburi cha hali ya juu kwenye kulinda maslahi mapana ya viongozi badala ya wananchi. Kiongozi wa ccm akiguswa hata kama kosa alilofanya lina uwezo wa kukidhalilisha chama kwa kiasi kikubwa atatetewa na kulindwa hata na jeshi ili asionekane amekosea. Mifano tunayo: waziri Malima alipotembea na bunduki ya kivita mpaka hotelini na ikaibiwa na anayesemekana ni "kimada" chama hakikuchukua hatua yoyote na badala yake anazidi kupaishwa. Majuzi Mh. Kapuya alipotajwa na kabinti kadogo kuwa alikuwa amekaambukiza magonjwa mabaya, hakuna kiongozi yeyote wa ccm aliyejitokeza hadharani na matokeo yake likatumika jeshi kupambana na vile vitoto ili kulinda maslahi ya wakubwa. na mifano mingine mingi ya jinsi hiyo. CCM Inaipeleka wapi nchi na wanataka tuamini wao ni nani?
1. Wanatupeleka wanakotaka viongozi na si wanakotaka wananchi na hii ni rahisi kushindwa kwani unaweza tu kumpeleka punda mpaka mtoni lakini si kumlazimisha kunywa maji. Jana nimesoma mahali aliyekuwa mkuu wa shirika la umoja wa mataifa la makazi na pia waziri wa ardhi akizungumza mambo yasiyo ya hadhi yake kuhusu katiba. Eti hakuna cha kuogopa kupiga kura ya siri bali kura zote ziwe na wazi. Hii ni dalili ya kutaka kuletea wanaopenda demokrasia vitisho vya waziwazi. Ukipiga kura ya siri hatutajua nani amesema nini na ni rahisi kuelezea msimamo wa waliokupeleka bunge la katiba lakini ukipiga kura ya wazi ni rahisi baada ya hapo kutengwa na jamii husika kuwa wewe si mwenzao. CCM wanataka hivyo ili kuwatishia wajumbe wake ambao naamini kuna wengi tu wanaopingana na msimamo wa chama chao usiokuwa na maslahi mapana kwa taifa letu.
2. CCM wanataka tuamini kuwa mawazo yao ni mawazo ya wananchi kwa kisingizio tu kuwa wao walichaguliwa na wananchi wengi. Sisi hatupingi sauala la ccm kuchaguliwa kwa uwingi wa kura na wananchi mwaka 2010. Lakini mara baada ya pale lazima chama kinachojali kuwa uongozi ni dhamana kirudi kwa waliokipa dhamana na kuwasikiliza na kuwahudumia. Kinyume cha hapo kuna kitu watawala wetu hawa wanapika na muda si mrefu kitapakuliwa mezani.
3. Lazima tufike mahali pa kuona kuwa katiba inayoandaliwa si ya wanasiasa na ya chama fulani cha siasa. Namkumbuka Mwenyekiti wa ccm wakati anakubali kuandikwa kwa katiba hii alisema "Tuwe na katiba itakayotuvusha kwenye miaka hii hamsini inayokuja". Naona kinyume na kauli ya kiongozi huyo ndiyo yanayofanyika huku yeye mwenyewe akiwa kimya bila kutoa wazo lolote. Ina maana amekubaliana na chama chake kinayoyataka na pia ameamua kulisaliti taifa kwa maslahi ya chama chake. Siku zinakuja hapa patakuwa hapatoshi wananchi watakapoamua kuwa wanataka yale wanayotaka na si yale viongozi wanayotaka. Hapo mwananchi wa kawaida hawataogopa tena FFU, JW na wala polisi au chombo kingine wala mtutu wa aina yoyote ile. Ni heri tutengeneze mazingira mambo hayo yasitokee. Kama tumeamua demokrasia twende na demokrasia, kama bado hatuitaki demokrasia tuseme waziwazi
 
teh.....teh......teh......teh......ccm bwana aaah wajanja sana, teh......teh......teh......mwe, ila siku zao naona sio nyingi sana, teh......teh.....teh.........teh........ eti kwenye katiba mpya wanataka uwazi, teh.....teh.....teh..... sasa nimejua ccm hawajiamini ndiyo maana wanataka uwazi kwenye katiba mpya......teh.....teh.......mweeeee ccm bwana eeeh wajanja kweli...teh.....teh........ wajameni.
 
Wana CCM tulijadili hili maana naona tunahitaji mwelekeo wa kisiasa.
Kwa mada hii hata CHADEMA hawajui end game ni ipi ilhali we are now travelling on uncharted waters.
 
teh.....teh......teh......teh......ccm bwana aaah wajanja sana, teh......teh......teh......mwe, ila siku zao naona sio nyingi sana, teh......teh.....teh.........teh........ eti kwenye katiba mpya wanataka uwazi, teh.....teh.....teh..... sasa nimejua ccm hawajiamini ndiyo maana wanataka uwazi kwenye katiba mpya......teh.....teh.......mweeeee ccm bwana eeeh wajanja kweli...teh.....teh........ wajameni.
Sijaelewa unacheka nini wakati huja dadavua mada!
 
Back
Top Bottom