Katiba Mpya - CCM yakataa Mapendekezo Matatu ya Tume ya Warioba

Katiba Mpya - CCM yakataa Mapendekezo Matatu ya Tume ya Warioba

Lengeri

Senior Member
Joined
Jul 3, 2009
Posts
180
Reaction score
17
1. Nec ya CCM imekataa suala la kuweka kikomo cha vipindi vitatu kwa wabunge. Badala yake imependekeza mfumo wa sasa wa bila ukomo kuendelee.

2. chama hicho kimekataa pendekezo la mawaziri wasitokane na wabunge na kutaka utaratibu wa sasa wa mawaziri kutokana na wabunge uendelee.

3. Kuhusu mfumo wa Muungano wa serikali tatu, CCM imepinga pendekezo hilo na badala yake kutaka mfumo wa serikali mbili uendelee kama ulivyo sasa.

Pendekezo ya Tume hiyo inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba ya kuwa na uwakilishi wa asilimia 50 kwa 50 katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wabunge wanawake na wanaume limekubaliwa na chama hicho tawala.

Source: Nipashe.

cc: Chama, Ritz, Pasco, Nguruv3

Lengeri watabana mwisho wataachia,wamezoea kutudanganya,eti wamekusanya maoni ya watu milioni mbili,wakati huku uswahilini hata vikao vyao hatuvisikii wala hatujui wanavifanyia wapi,sijui wanafanya na wake zao chumbani?,Yaani magamba ni wahuni na matapeli watupu!
 
Last edited by a moderator:
walikuwa wanatoa na sababu za kukataa kwao ama walijua tu kukataa?
 
Kila mtu anauhuru wa kutoa mawazo yake au maoni yake ni mawazo mazuri inategemea undani wake upoje.
 
Lengeri watabana mwisho wataachia,wamezoea kutudanganya,eti wamekusanya maoni ya watu milioni mbili,wakati huku uswahilini hata vikao vyao hatuvisikii wala hatujui wanavifanyia wapi,sijui wanafanya na wake zao chumbani?,Yaani magamba ni wahuni na matapeli watupu!
Wewe si ulikuwa kwenye mikutano ya hadhara hivyo bikao utaviona wapi bavicha bwana.
 
1. Nec ya CCM imekataa suala la kuweka kikomo cha vipindi vitatu kwa wabunge. Badala yake imependekeza mfumo wa sasa wa bila ukomo kuendelee.

2. chama hicho kimekataa pendekezo la mawaziri wasitokane na wabunge na kutaka utaratibu wa sasa wa mawaziri kutokana na wabunge uendelee.

3. Kuhusu mfumo wa Muungano wa serikali tatu, CCM imepinga pendekezo hilo na badala yake kutaka mfumo wa serikali mbili uendelee kama ulivyo sasa.

Pendekezo ya Tume hiyo inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba ya kuwa na uwakilishi wa asilimia 50 kwa 50 katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wabunge wanawake na wanaume limekubaliwa na chama hicho tawala.

Source: Nipashe.

cc: Chama, Ritz, Pasco, Nguruv3

Duh hapo kwenye red, ni kiwewe cha nafasi yao Kisiasa, wanajua kabisa hali halisi, ila kile kitendo cha CHADEMA kutangaza position yao kuhusu hili, imewachanganya sana. Ninaongea nao wengi wa Viongozi wa CCM, bado hawana hoja nzito ya msingi na cha ajabu wenyewe hawaamini msimamo huo, ni kituko kweli.

kinachonishangaza ni kitendo chao cha kufumbia macho taarifa za kiitelijensia zinazoonyesha kuwa kuna shinikizo kubwa la Zanzibar kudai Mamlaka Kamili, na shinikizo hilo lilipelekea wao kuanza kuchukua hatua kuanza kuweka mazingira ya kupata mamlaka kamili. Tayari Zanzibar ina Katiba, Bunge, Rais, Bendera na Wimbo wa Taifa. Serikali ya Muungano inasita kulizingimzia hili. Iwapo chochote kitatokea kwa Katiba Hii kupita, hoja kubwa itakuwa ni kama itakidhi matakwa ya Katiba ya Zanzibar.

Kituko kingine ni kutudangaya kwa kutuambia serikali ya muungano ni ya serikali mbili wakati ni muungano wa serikali moja tu, na kimantiki serikalinyingine inayoungana nayo haipo. Hata kichaa anaweza kuliona hilo. Muungano unaozungumziwa na kuuzwa na CCM katika lugha na tafsiri ya kawaida neno "Muungano" wanalitumia vibaya na hapa ni kutudangaya. Serikali ya pili inayopaswa kuungano na yo haina bunge, haina katiba yake, haina rais, ni basi tu navingine vingi vinavyunda serikali kamili.
 
Wanafikiri watanzania wanataka kutengeneza katiba ya kijani ya zidumu fikra za mwenyekiti.
 
Lbda sielewi ccm ni nani; kama ccm wanachama wote wa ccm basi huo si msimamo wa ccm, kama ccm ni viongozi wa kamati kuu basi huo ni msimamo wa ccm. Mtu wa kwanza kukataa serikali tatu alikuwa Nape kwa nafasi yake kama katibu wa itikadi hata kabla kamati kuu haijakaa. Kamati kuu ilipokaa ikasema ccm haikubali serikali tatu na watawaelekeza wanachama wao wazikatae serikali tatu. Kwa maana hiyo huo ni msimamo wa viongozi ambao umepandikizwa kwa wanachama wao. Wakumbuke kuwa wakati wa kutoa maoni binafsi kwenye tume, wanachama haohao mmojammoja bila kushawishiwa na viongozi ndio walisema serikali tatu.
Je haya ya sasa si ya viongozi tu?

Jaji Warioba alishawaambia, haya waliyoandika kwenye rasimu ni maoni ya wananchi kinachotakiwa ni kuyaboresha si kuyafuta!
 
Back
Top Bottom