Katiba mpya haina suruhisho la matatizo ya watanzania

Katiba mpya haina suruhisho la matatizo ya watanzania

Joined
Sep 24, 2013
Posts
33
Reaction score
6
Matatizo yanayotukabili watanzania kwa kiasi kikubwa ni zao la katiba mbovu tuliyonayo. Katiba hii inawapa mamlaka makubwa na kinga kubwa sana watawala wetu kiasi wanakuwa kama miungu mbele ya kundi kubwa la watawaliwa.
Mfano,ibara ya 46- (2) inasema,`Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii,itakuwa ni marufuku kumshitaki au kuendesha mashitaka ya aina yoyote juu yake mahakamani kwa ajili ya kosa lolote alilolitenda au alilokosa kulitenda yeye binafsi kama raia wa kawaida ama kabla na baada ya kuwa Rais'.Kipengele hiki nd'o chimbuko la matatizo yote sugu (kama vile kukithiri kwa rushwa/ufisadi kama vile: KIWIRA, EPA,RICHMOND,BoT, MEREMETA,RADAR,n.k.Pamoja na kukithiri kwa vitendo vya ujangili, biashara ya `unga',utekaji,utesaji na mauaji ya raia wasio na hatia kwa tindkali,risasi na mabomu) ambayo yanaliangamiza taifa hili,watu wake na raslimali zake.
Mytake: Katiba Mpya imuondolee Rais kinga ya mashitaka na awajibike moja kwa moja kwa wapigakura sawa na mbunge.
 
Back
Top Bottom