Katiba mpya haitapatikana kwa tabasam tutarajie minyukano na huu ndo ukomavu

Katiba mpya haitapatikana kwa tabasam tutarajie minyukano na huu ndo ukomavu

twijuke

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2011
Posts
547
Reaction score
252
Watanzaia wenzangu wana jukwaa poleni na majukumu.

Watanzania wengi pamoja na jukumu la kuusaka mkate lakini macho yetu masikio viko Dodoma, katika ufuatiliaji wetu mitaani na kwenye mitandao ya kijamii tumekuwa na mitazamo tofauti, wako wanaoona kuwa kwa jinsi watu wanavyo tofautiana kuwa nchi inaelekea kubaya na hawa ndo wengi, na wako wanaoona kuwa ni sahihi. Ukweli unabaki kwamba kwa jambo zito namna ile ni vigumu vichwa zaidi ya 600 kuwa na mawazo sawa, tukumbuke kuwa pamoja na wingi wao bado wametofautiana makundi mbali mbali, kuna wanao unga mkono hoja rasimu ya pili ya katiba ambayo imebeba maoni ya wananchi, zaidi aya asilimia 60 tunaambiwa wanataka serikali 3. Lakini pia upande mwingine ni wale wanaotaka serikali 2.

Kwa mtazamo wangu si jambo jepesi watu wenye mitazamo tofauti kutekeleza jambo zito namna ilie kimaamuzi huku wakiwa wamejawa na nyuso zenye tabasam. Tutarajie minyukano na huu ndo ukomavu. Mfano ccm wawmeingia kwenye bunge la katiba wakiwa wamejitanabahisha kuwa msimamo wao ni serikali 2, hivyo tusishangae kutumia kila mbinu za aina mbalimbali kuhakikisha wanapata uungwaji mkono kwa msimamo wao wa serikali 2, tunao piwa hawa wa vyama vya upinzani ambao wamejipambanua kuwa wao wana linda maoni ya wananchi kuhakikisha maoni yao ya serikali 3 yanapita, hawa nao tutarajie kuona wakitumia mbinu na mikakati mbalimbali kuhakikisha serikali 3 inapita, mfano kwa mjibu wa ratiba ya shuguli za bunge la katiba ilikuwa Rais azindue bunge la katiba na badaye mwenyekiti wa tume ya katiba Jaji Warioba aje kukabidhi rasimu ya pili ya katiba.

Lakini kwa taarifa zisizo rasimi, inaonekana ccm kwa msimmamo wao wa serikali2 waliamini kuwa endapo Rais atazindua bunge la katiba kwanza na badaye warioba akija kukabidhi rasimu ya katiba atamwaga kilichodhaniwa kuwa ni sumu, hivyo wakafanya mkakati ili Warioba akabidhi rasimu kwanza, na badeye afuate Raisi kwa maana ya kufuta nyao na kubomoa kilichojengwa na Warioba kwenye vichwa vya wajumbe wa bunge la katiba. Baada ya wajube kubaini mkakati huu uliodhaniwa kuwa ni wa ccm ndipo tuliposhudia kwa mara ya kwanza Warioba anashindwa kuhutubia baada ya baadhi ya wajumbe kuwa wamejiratibu kuzomea wakiwa na lengo la kuhakikisha Warioba hahutubii. Kama tulivyo shuhudia lengo la wajumbe hawa wapinzani lilitimia baada ya mwenyekiti wa bunge kuliahirisha bunge na badaye kamati ya mashauriano na maridhiano walikaa na kuamua Warioba ahutubie siku iliyofuata, kumbuka awari Warioba alikuwa ametengewa masaa mawili sawa na dakika 120, lakini baadaye kamati ya maridhiano wakaamua kwakuwa atakapoanza ahutubie mpaka amalize. Pamoja na lawama walizo shushiwa wapinzani, wote tu mashahidi wa kazi nzuri ya uwasilishaji wa rasimu ya pili katika bunge la katiba imefanikishwa na wapinzani, kwani masaa mawili aliyokuwa ametengewa mzee Warioba na mwenyekiti wa bunge yasingetosha.

Ni katika mazingira haya ya mikakati ya pande zote mbili jinsi watu wanavyotofautiana na hatimaye kuweka mambo sawa,watanzania wenzagu tutarajie mengi, wakati mwingine hata ngumi na pengine hata baadhi ya wajumbe kutishia kuondonka, nawasihi sasa tuanze kuzoe marumbano mabishano, na mikwaruzano, mambo yote haya ndo yatajenga kuheshimiana.
 
Back
Top Bottom