Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Habari ya karibuni kabisa ni Serikali kuchukua mkopo toka South Korea kiasi cha dola bilioni moja.
Kuchukua mkopo kwa nchi siyo jambo baya na wala siyo jambo la ajabu. Tatizo lipo kwenye matumizi. Unachukua mkopo kufanyia nini? Sababu uliyochukulia mkopo ina impact gani ya haraka ya kulipa mkopo.
Baba anayejitambua, kukopa pesa ili ukanunue ardhi ili ufanye kilimo, uzalishe, itaeleweka. Ila kuchukua mkopo ukanunue blanketi ya kujifunika na mkeo ni aibu kubwa.
Eti sehemu ya pesa ya mkopo tuliochukua toka South Korea, inaenda kutumika kutengeneza vitambulisho vya Taifa na kufanyia sensa ya ardhi.
Tunakopa fedha kufanyia vitu ambavyo tulistahili kuvifanya wenyewe. Ni sawa na baba wa familia anayekopa kwaajili ya kunua shuka au blanketi la kujifunika na mkewe.
Kama tunashindwa hata kuwa na pesa ya kutengenezea vitambulisho vya wananchi wetu, hivi sisi tunaweza kitu gani? Hizi pesa zinazokusanywa kwa kwa kupitia kodi msululu, zinashindwa kutengeneza hata vitambulisho tu? Pesa zetu zinatosha kununulia tu V8 za viongozi na za kulipia misafara na safari za viongozi tu?
Tupate katiba mpya. Na ndani ya katiba mpya, iwekwe wazi kuwa mikopo ya Serikali itakuwa ni kwaajili ya miradi ya maendeleo tu inayohusisha ujenzi wa barabara, reli, njia za umeme, usafiri wa anga, majini na nchi kavu, ujenzi wa mabwawa ya umwagiliaji, usambazaji wa maji, na ujenzi wa hospitali maalum. Serikali isikope hela kwaajili sijui ya mafunzo, kujenga mifumo, n.k. Ni matumizi mabaya ya pesa za mikopo.
Pesa za mikopo ziende kwenye vitu vinavyoonekana wazi, na vina impact ya moja kwa moja kwa maendeleo na maisha ya wananchi na Taifa. Mambo ya eti ujenzi wa mifumo, mafunzo, semina, ni lazima tutumie pesa zetu za ndani.
Kama Taifa, ni lazima tuwe na mambo ambayo tunaweza kusema, HAYA TUNAWEZA NA TUTAYAFANYA KWA PESA YETU WENYEWE, na yaliyobakia tunaweza kukopa na hata kuomba misaada, ikilazimu.