Katiba Mpya imefanya Mapinduzi ya Kiuchumi, Kenya imezipiku Mapato ya Tanzania, Uganda na Rwanda kwa Pamoja

Bush Dokta

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2023
Posts
24,831
Reaction score
45,154
Kanuni ni zile zile kwenye uchumi na hata kwenye maisha ya kawaida.

Ili ujenge uchumi wako mfukoni unahitaji kukusanya mapato, kubajeti matumizi na kidhibiti upotevu na matumizi holela ya Fedha zako mwenyewe.

Kwenye upande wa kudhibiti matumizi na kuhakikisha hakuna ukwepaji wa kodi, upotevi wa fedha na hata matumizi mabaya ya fedha za Umma Kenya inang'ara.

Chanzo za mafanikio makubwa Kenya ni Katiba Bora waliyopigania kwa miaka mingi. Katiba inayohakikisha kila mtu anaogopa kupiga fedha za umma.

Ni katiba ambayo inahakikisha Rais aliyeko madarakani hawezi kuwalinda wezi, wala rushwa, maswahiba wafanya biashara wasiowazalendo.

Zaidi ya haya ni kuwa NIS inawezeshwa kufanya kazi kwa ufanisi Mkubwa ikishirikiana na vyombo vingine kama Mahakama, Polisi, Jeshi la Ulinzi na Magavana wa kaunti mbali mbali.

Haiingii Akilini Nchi ndogo kama Kenya yenye Idadi ya Watu 50M inazalisha Mapato zaidi ya watu 120M combined.

Hivi ni vichekesho tena badala ya kuwaonea wivu na kuwachukia tunapaswa kujifunza kwao.

Kenya 1.jpg

Kenya Ni miongoni mwa Nchi za Afrika mashariki zilizoondoa woga na kujikita kwenye Demokrasia ya kweli. Ingawa bado sio demokrasia kamili na bado ina mapungufu lakini bado ni bora zaidi ukilinganisha Tanzania ,uganda, rwanda na Burundi.

Nchi ya Kenya sasa kuna utulivu, hakuna Chaguzi za marudio zinazotokana na watu kuunga juhudi.

Nchini Kenya Watumishi wa Taasisi za Umma huteuliwa kwa mrengo wa Uwezo, uzoefu, weledi na Uzalendo na sio kwa sababu ya Mapenzi au uanachama wa chama fulani.

Kwa hili kenya imepiga hatua kubwa na itazidi kupaa siku hadi siku.

Tujitafakari sana.
 
Uchumi wa kenya unakuwa kwa kasi ya 5.9% mwaka 2021 na Tanzania 5.2% kwa mwaka 2023.
 
Kwetu tunaamini kwenye mikopo na misaada hayo mengine ya kwao, kila nchi na njia zake.
 
upotevi wa fedha na hata matumizi mabaya ya fedha
☝🏿
Fedha za michango ya "Join the chain" za wana CHADEMA hazina maelezo yakuridhisha, yaani hazijulikani zimeenda wapi. Je ni kwasababu za Katiba ya CHADEMA kuwa ya zamani?
aliyeko madarakani hawezi kuwalinda wezi, wala rushwa, maswahiba wafanya biashara wasiowazalendo.

☝🏿Nani huyo, Mbowe? Tumesikia rushwa zilizotamalaki katika chaguzi zenu, Je, Katiba yenu hailindi rushwa huko?
 
Katiba Mpya imefanya Mapinduzi ya Kiuchumi, Kenya🤔😮​

Yaani Mada inasema Kariba mpya imefanya Mapinduzi ya kiuchumi, na katika maoni yako unadai👇🏿
Chanzo za mafanikio makubwa Kenya ni Katiba Bora waliyopigania kwa miaka mingi. Katiba inayohakikisha kila mtu anaogopa kupiga fedha za umma.
....halafu post hiyo ya X inasema..."Licha ya bajeti yao ya mabiloni ya Dola, bado wana kiwango cha juu zaidi cha ukosefu wa ajira, gharama za kufanya biashara ni kubwa zaidi kulinganisha na na nchi zilizomo katika kand aya Afrika Mashariki-Tanzania included.

Hiyo☝🏿 juu tunaweza kusema kwa uhakika kabisa kwamba
  • Unapotosha Umma
  • Katiba yao "Mpya" haijafanya hayo mapinduzi ya kiuchumi kama unavyotaka kutuaminisha- unavyodai
  • kwamba
pamoja na Katiba yao mpya, umasikini, ukosefu wa ajira na gharama zingine kubwa zimetamalaki kuishinda Tanzania yenye Katiba hiyo mnayodai imepitwa na wakati🙌🏾

Yaani Tanzania na nchi zingine za kanda hii, kuna ubora wa maisha, umasikini upo chini, tuna kiwango kidogo cha ukosefu wa ajira, na gharama za kufanya biashara ni nafuu kuliko huko Kenya-licha ya kuwa na Katiba ya "zamani"

Itoshe kusema, hakuna sehemu yoyote ile kwenye hilo bandiko la X linaposema "Ni Katiba ndio imeifanya Kenya kuongoza kwa kukusanya Mapato makubwa"-Hakuna

Wewe umetoa wapi Katiba mpya imefanya mapinduzi ya kiuchumi Kenya?
(Maoni yako yanazingatiwa)

Naona CHADEMA mmeishiwa, na kama kawaida yenu, mnaendelea kupotosha umma, kwa kuunga unga mambo yasiyo na kichwa wala miguu. Yaani Uwasilishaji wenu wa Taarifa umekumbwa na Ulaghai na hadaa. Ati Katiba mpya imefanya mapinduzi.

Yote hayo kwasababu za kusaka madaraka. Uraisi.

Nafikiri itakuwa sahihi kusema CHADEMA ndio mnaohitaji KATIBA mpya ya Chama cha kumuondoa Nduli Freeman Mbowe-mnahitaji Katiba mpya kuleta mapinduzi kwenye chama chenu(muonyeshe mfano) halafu ndio mje kudai KATIBA mpya.
 
Asante kwa kuchangia karibu tena
 
Back
Top Bottom