Katiba Mpya ina umhimu gani kwa raia maskini Tanzania

Katiba Mpya ina umhimu gani kwa raia maskini Tanzania

hermanthegreat

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2021
Posts
1,274
Reaction score
3,282
Habari Jf
kumekuwa na movement nyingi za kudai katiba mpya Tanzania mitandaoni.
Naskitika kugundua kuwa watu wamekosa vitu vya kudai kabisa hadi wanaanza kulilia katiba mpya.
Pengine mimi sielewi.
Katiba mpya[emoji116]

[emoji117]Inasaidiaje kutatua tatizo la ajira Tz

[emoji117]Inamsaidia nini bibi aliye kijijini (hakuna umeme, maji, kiufupi social services hazipo)

[emoji117]Ina umhimu gani in general katika kusaidia wananchi maskini.

asanteni. Karibu kwa hoja(iliyoshiba)
 
Kweli wewe huelewi na hujui kama huelewi, manake umeisha tanguliza maneno ya "kwamba wamekosa vitu vya maana vya kudai".
 
Elimu yako kwanza ni vizuri uiweke wazi ili wakija watu kutoa comments zako wajue wanaongea na mtu mwenye elimu gani?
 
yaani wanataka zitumike temna mamilioni kutengeneza hayo makaratasi hayana umuhimu tutumie ya sasa haina shida
 
Kila inapotajwa katiba mpya, basi huambatana na maneno "tume huru". Haihitaji akili kujua mnufaika mkuu ni nani, na anasisitiza hili jambo kwa manufaa gani.
Wananchi wa kawaida hiyo katiba wala sio ajenda yao.
 
Umasikini au utajiri hauletwi na katiba ndio maana hata kwenye hii kuna maskini wakutuwa na matajiri wenye kufuru zao.

Ila umuhim wakuwa na Katiba mpya bado upo palepale, kwa sababu ndio sheria mama yakutuongoza tuishi vp katika nchi yetu.

Sasa basi katika hii iliyopo kuna mengi ambayo hayako sawa ktk ulimwengu wa kizazi hiki hivyo kuleta sintfaham katika mazingira mengi hasa ya watawala na watawaliwa au viongozi na wanaoongozwa.

Uzi wako umejikita katika kupinga umuhim wa katiba mpya kwa hoja za kimasikini utadhani wanaohitaji ni masikini au inahitajika kumsaidia masikini ppekee.

#Katiba Mpya Ni Lazima itapatikana... maana walioipitisha iliyopo wamebaki wachache sana kuliko sisi tulioikuta. Tunataka Katiba inayshabihiana na malezi makuzi mazingira na utandawazi tunaoishi nao.
 
Umuhimu wa katiba mpya ni kuwa mifuko ya Hifadhi, hasa sekta binafsi NSSF ni kusimamiwa na vyama vya wafanyakazi

FAO LA KUJITOA ili vijana wanaotaka kutumia intellectual property zao kubuni miradi yao, na kuongeza wigo wa Kodi kwa Taifa.

Pili, Bima ya afya kuwa na viwango vidogo vya afya ili masikini wanyonge wengi waingie
 
Back
Top Bottom