Habarini za humu ndani ndugu zangu
Mimi kama ni mwana Jamii Forom, tena mwenyeji wa muda mrefu sana humu ndani, naomba nami nichangie mawazo yangu hasa kwenye Tanzania tuitakayo kwa ajiri ya kizazi kilichopo na kijacho.
1. Katiba mpya itaweza kuja na mwarobaini hasa kwa Rais aliyepo madarakani, ikitokea amefariki dunia, Katiba ya sasa hivi inasema Makamu wa Rais ndiyo atakua Rais hadi pale kipindi cha Rais aliyefariki kutamatika,mfano kama ilikua imebaki miaka 3, basi Makamu wa Rais atakua Rais hadi miaka mitatu iish. Hii nasema Hapana.
2. Nasema hapana kwa sababu zifuatazo
i)Makamu wa Rais anaweza fanya sabotage kwa Rais,akampindua au akapanga mipango yakutoa uhai wa Rais aliyeko madarakani,sababu anajua kwamba atakua Rais, hii napendekeza kwamba, Rais akifariki dunia akiwa madarakani, Makamu wa Rais ashikirie nafasi ya Rais kwa kipindi cha miezi 2, siku sitini tu, na uchaguzi mpya ufanyike kupata Rais mpya.
ii) Makamu wa Rais akipata nafasi ya Rais anakua hajajiandaa kimwili,kiakili na kisaikolojia, ndiyo maana wakati mwingine anaweza shinda timimiza majukumu yake na kusingizia kwamba alipata nafasi ya Urais bila yakujipanga.
iii) Ratiba yetu itamke kwamba ni marufuku kumusifia,kumtukuza Mh Rais aliyepo madarakani, Katiba yetu itamke ni kosa la jinai kuwa Chawa wa kiongozi flani, iwe kuanzia nafasi za juu hadi nafasi za chini kabisa
iv) Katiba yetu itamke kwamba kila mwanachi ana haki ya kuishi,inapotokea mtu flani kapata matatizo kutokana na vitisho vya mtu au watu, basi hao watu wachukuliwe sheria kali kabisa.
v) Kila kijana anapotoka Chuo Kikuu,basi aweze kupata nafasi ya kushindana kwenye usaili wa nafasi mbali mbali, kila mtu apatiei usaili na sio kuwa kwamba, baadhi ya vijana wanapata kazi kwa kupitia migongo ya ndugu zao.
vi) Nafasi za teuzi ziwe zinafanyika kwa njia ya usaili,hii itafanya mtu anayepata kazi kufanya kwa nguvu zake zote na sio kufanya kazi kwa kusifia mtu aliyemteuwa ili kulinda kibarua chake.
vii) Ni marrufuku kwa kiongozi yoyote kuwa na mali nyingi sana ambazo kazipata ndani ya muda mfupi tu,toka ateuliwe kuwa kiongozi wa taasisi ya serikali.