Katiba mpya isiwe chanzo cha uvunjifu wa amani

Joined
Mar 7, 2015
Posts
21
Reaction score
1
UZURI WA KATIBA INAYOPENDEKEZWA NI ZAIDI YA MAPUNGUFU YALIYOMO: MAKALA NO. 2 Katiba inayopendekezwa imepitia mchakato mpana wa ushirikishwaji wa wananchi wa kada mbalilmbali hivyo haina shaka kwamba katiba mpya itapatikana kidemokrasia. Watanzania wote tunahitaji katiba mpya pamoja na tofauti chache zilizopo miongoni mwa wadau wa katiba hasa vyama vya siasa.

Kwa kiasi kikubwa katiba inayopendekezwa imekidhi matakwa yasasa ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni kama inavyojidhihirisha katika ibara ya 11,12,13,14 na 15 ambapo kwa mara ya kwanza nchi yetu inakuwa na malengo ya kitaifa yaliyoainishwa ndani ya katiba nahivyo kusimamiwa na katiba ambayo ndiyo sheria mama ya nchi. Malengo hayo ya kitaifa yanaathiri mojakwamoja maisha ya watanzania. Kwahiyo tunapoijadili katiba mpya nivema tukaiangalia kwa kuihusianisha na maisha ya watanzania kuliko matakwa ya kisiasa.

Tanzania ni nchi yetu sote tuliohai kwa sasa pamoja na vizazi vyetu vijavyo hivyo upo umuhimu wa wadau wakatiba kutafakari vema iwapo harakati zao za kisiasa kuhusu katiba mpya zinamanufaa kwa wananchi wote au makundi Fulani kwa kutumia mgongo wa watanzania. Ni vizuri mchakato wa kuipata katiba mpya ukazingatia maslahi ya watanzania wote bila kujali tofauti za kisiasa, kidini,kikabila, na hata kijamii ili mwisho wa mchakato huu watanzania tubaki kuwa wamoja nakushirikiana kuijenga nchi yetu. Kwa wingi wetu, makundi nimengi na mahitaji nimengi ila siyo lazima kila hitaji la kundi Fulani liwemo kwenye katiba isipokuwa jambo muhimu la kuhakikisha nikwamba maslahi yote yalindwe na katiba. Yapo mambo ambayo yanaweza kufanywa na kundi Fulani kwa maslahi ya kundi hilo bila kukiuka sheria za nchi na jamii ikawa salama.

Nivizuri ifahamike kwamba kwa wakati tulionao katika bara la Afrika ni Tanzania pekee ambayo inawingi wa makabila pamoja na watu wengi wenye tofauti za kiimani lakini wanaoishi kwa umoja wahali ya juu. Hali hii lazima inawatamanisha maadui waliojificha kuvunja amani ya nchi hii na mlango wa kuingilia nikuwatumia watanzania wenyewe.

Nichukue furusa hii kuwaomba wanasiasa wote pamoja nawatanzania kwa ujumla wetu tuuchukulie mchakato wa katiba mpya kuwa niwetu sote na siyo wa kundi Fulani hasa wanasiasa wanaoonekana kutaka kuhodhi mchakato huu. Tukiwa na fikra hizi itakuwa rahisi kutulia na kuisoma katiba inayopendekezwa kisha kuchukua uamuzi wa kuikubali au kuikataa bila ya kuwa na ushawishi mkubwa kutoka kwa wanasiasa.

Mazingira ya Tanzania nawatanzania lazima yatazamwe katika kuijadili katiba pendekezwa. Tusiijadili katiba pendekezwa kwa kuhusianisha sana katiba yetu na katiba za mataifa mengine bila shaka mazingira yanchi yetu nitofauti nayanchi nyingine ingawa yapo mambo machache yanayoweza kuigwa na kufananishwa na katiba za nchi nyingine. Kinachotakiwa hapa ni wadau wa katiba kuwa wakweli na waadilifu katika kuwaelimisha watanzania juu ya katiba inayopendekezwa. Kauli za kujenga uhasama miongoni mwa watanzania na kusambaratisha umoja wetu kwa hoja ya kuitaka katiba mpya siyo sahihi kabisa na inafaa kuziacha kama kweli lengo nikuwapatia watanzania katiba na siyo kuvipatia vyama katiba.

Katika jumla ya ibara 296 zilizomo katika katiba inayopendekezwa takribani ibara zote ninzuri ingawa kuna mapungufu machache ambayo kwa mwono wangu hayaifanyi katiba inayopendekezwa kukosa uzuri wa kukubalika. Ifahamike kwamba hii nimara yakwanza kwa nchi yetu kutunga katiba ya kidemokrasia yenye ushiriki mpana wa wananchi hivyo mapungufu machache hayawezi kukosekana kwa kuwa katiba hii haikutoka kwa mungu, imetungwa na wananchi ambao wana matakwa ya kibinadamu hata misingi ya imani ya dini zetu inatwambia kwamba tutaingia peponi au motoni kwa wingi au uchache wa matendo mazuri ambayo mungu anayaridhiwa. Hii inatufundisha kwamba hakuna binadamu mwenye uwezo wakuwa msafi kwa asilimia zote muhimu ubaya usiwe mwingi kuliko uzuri.

Ukilinganisha katiba pendekezwa na ile ya 1977 inayotumika sasa nidhahiri kwamba katiba pendekezwa inatoa mwanga zaidi kwa watanzania kufanikiwa kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kijamii kuliko ile ya 1977. Nikiwa mdau anayependa katiba pendekezwa ikubalike kwa watanzania, ninakiri kwamba yapo mapungufu machache sana ambayo nina amini hayawezi kuwa hoja za kukwamisha kupatikana kwa katiba mpya kama kweli tunadhamila ya kuipata katiba mpya kwa manufaa ya watanzania.

Tusikubali kurudi nyuma, twende mbele kwa kuikubali katiba mpya na baada ya hapo tuanze kufikiria kurekebisha haya mapungufu machache yaliyomo. Katiba siyo msahafu usiobadilika, ni matakwa ya watu na watu ndio sisi. Mabadiliko makubwa ya haraka huwa yanamatatizo kwa umma. Sikubaliani kabisa na kauli zinazotolewa kwamba katiba hii pendekezwa ni mbovu na haifai.

Haki za binadamu zilizomo katika katiba pendekezwa zimelindwa vizuri kikatiba na haki za binadamu ndiyo msingi mkuu wa utoaji huduma kwa serikali dhidi ya wananchi wake. Hili ndilo eneo muhimu sana kuliko mambo menngine katika katiba yoyote, upana na ulinzi wa haki za binadamu ni muhimu kuliko maslahi mengine ya kisiasa ambayo ndiyo msingi wa wanasiasa wengi kutofautiana katika mchakato huu wa kuipata katiba mpya. Katiba hii imetambua na kulinda haki nyingi sana za binadamu ambazo watanzania wengi tunazihitaji kuliko masuala ya kisiasa zaidi ambayo kwa mwono wangu katika wengi wanaoikataa katiba mpya wana ajenda ya maslahi ya kisiasa zaidi kuliko yakwetu wananchi.

Suala la mbunge kuwa waziri na Rais kuwa sehemu ya bunge ni baadhi ya maeneo madogo yanayoibua hoja na hayana madhara sana kwa maendeleo ya Taifa na wananchi ikizingatiwa kwamba kwa mujibu wa ibara ya 115(2) ya katiba pendekezwa idadi ya mawaziri na manaibu waziri wa serikali ya jamhuri ya muungano hawatozidi arobaini. Hii ni idadi ndogo ya jumla ya wabunge wote ambayo haiwezi kudhoofisha nguvu ya bunge katika kuamua mambo ya msingi.

Vilevile ifahamike kwamba bunge katika kutenda majukumu yake na kuhakikisha linaisimamia serikali ibara ya 158 (1) bunge lina mamlaka ya kuunda kamati za bunge za aina mbalimbali kwa ajili ya utekelezaji wa madaraka yake ambapo utendaji wa mawaziri unaangaliwa na kamati hizi za bunge kwahiyo mbunge kuwa waziri haina kwamba utendaji wa bunge unapungua isipokuwa hili tuliangalie katika mukhtadha wa mbunge ambaye niwaziri kama anaweza kuwa na muda wa kuwadumia wananchi wake kwa ufasha.

Ufanisi wa mbunge kuwajibika hautokani na mbunge kuwa jimboni mwake muda mwingi ila ni uwezo wa mbunge kutatua changamoto zilizomo kwenye jimbo lake kwa namna mbalimbali ambayo inafaa. Hoja ya kwamba Rais kuwa sehemu ya bunge inaathiri utendaji wa bunge na inaingilia bunge na kutokuwepo kwa mgawanyo sahihi wa madaraka katika mihilimili mitatu ya serikali siyo kweli.

Ni vizuri tukafahamu kwamba mihimili ya dola ni bunge, utawala na mahakama. Rais siyo mbunge na hana mamlaka juu ya bunge kuhusu utendaji wake. Mihimili hii haiwezi kutenganishwa kabisa bila kuhusiana katika utendaji kazi na utendaji kazi siyo kuingiliana. Hakuna serikali duniani ambayo mihimili yake inafanya kazi bila kushirikiana. Tafsiri ya mihimili ya dola kuwa huru nikila muhimili kufanya kazi yake bila kuingiliwa na muhimili mwingine kiutendaji na siyo kutoshirikiana kama inavyotafsiriwa na baadhi ya watu. Kuna tofauti ya kushirikiana na kuingiliana.

Rais ni mkuu wa utawala katika nchi hii haina maana kwamba anaingilia mihimili mingine isipokuwa hayo ni madaraka anayotekeleza Rais ambayo kwa asili yake hutekelezwa na mkuu wa nchi. Dhana ya mihimili kuingiliana ni pale ambapo muhimili mmoja unafanya kazi ya muhimili mwingine yaani uwepo wa mgongano wa majukumu yanayofanana katika mihilimili ya serikali, Rais siyo muhimili wa serikali, ni mtu na mihimili ya serikali siyo mtu ni vyombo. Tena Rais ni mkuu wa muhimili mmoja miongoni mwa mihimili mitatu ya serikali ambao ni utawala (Executive) na siyo mkuu wa bunge wala mahakama. Mkuu wa bunge ni spika na mkuu wa mahakama ni jaji mkuu. Kazi anazofanya Rais katika mihimili hii ni zile ambazo kwa asili yake hutekelezwa na mkuu wa nchi.

Katika utengenezaji wa katiba kote duniani pamoja na shuguli za serikali nisahihi kwa kila muhimili kuwa na majukumu ambayo yanatekelezwa na mkuu wa nchi na hapa ndipo tunapata maana sahihi ya mkuu wa nchi. Rais kama mkuu wa nchi hawezi kuwa na madaraka sawa na spika au jaji mkuu. MWANASHERIA MWESIGWA ZAIDI SIRAJI 0784 646220
 
Mchumia tumbo!
 
Back
Top Bottom