Tuko Watanzania milioni 60 hajuna uwanja unaoweza kutushikilia wote tukae tusainiane makubaliano yaani Katiba. Ingekuwa tuko wachache au ingekuwa ni kitu kimoja tukakubaliana sote 100% pia ingekuwa rahisi. Kwa vile tuko wengi na tuna mawazo tofauti, njia pekee ni kutumia wawakilishi tulipwachagua. Wawakilishi hawo ni Wabunge aina 3: Mbunge mmoja tumechagua kila jimbo la uchaguzi; Mbunge mmoja mmoja tumechagua kwa kila Kata (huyu huitwa Diwani); na Mbunge mmoja tumechagua kwa Nchi nzima (huyu huitwa Rais). Hawa ndiyo wana madaraka ya kutusema, watched wakae walete Katiba pendekezwa sisi Wananchi tupoge kura referendum. Tunakosea sana kuwadharau hawa kwa kuwaita "wanasiasa" kwa sababu hawa ni wateule wetu kwa kazi kama hizi. Hii ya kudai eti kuna makundi mengine kama wavivi au wamachinga au Wahandisi au Walemavu nk nk haina mshiko kwa sababu wite hawa wanawakilishwa kupitia majimbo yao (Mbunge), Kata zao (Madiwani), au Nchi yote (Rais). Mbona wengi ni CCM? Hakuna taabu, ndivyo Wananchi walivyochagua, lazima waheshimiwe. La sivyo mtu atasema mbona wengi ni weusi hakuna Wazungu? Mbona wote wanaongea Kiswahili hakuna wanaoongea Kifaransa? Mbona hakuna Wageni? Mbona hakuna Wahindu? Tutachoka, tuliochagua kwa hiari yetu wanatosha - yaani Rais, Wabunge na Madiwani. Tuwaachie.