Mmoja wa wachangiaji katika Kongamano la Katiba lilioendeshwa na Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA) mwishoni mwa wiki mkoani Katavi amedai:
"Kama katiba inatambua umri wa mtu kuoa na kuolewa kwamba miaka 14 kwa miaka 18, basi iwekwe ukomo kwa mtu kuolewa na kuoa kwasababu tumekuwa na taifa lenye vijana wa kiume, wengi wanakwepa majukumu, hawataki kuoa ila wanazalisha watoto wa watu"