Ngongoseke
JF-Expert Member
- Jan 1, 2012
- 3,202
- 1,462
Habari zenu wa jukwaa, kutokana na matatizo yanayoendelea ndani ya nchi yetu, mimi kwa maoni yangu naona bora katiba mpya izuie kabisa viongozi wa dini kujiingiza kwenye siasa au kushiriki mambo ya siasa wabaki washauri tu, nadhani hili litawajengea heshima kubwa katika jamii kuliko haya tunayo yashuhudia kwa sasa,
Na nina imani itasaidia sana kurudisha imani ya nchi ambayo ukweli ipo ICU.
Na nina imani itasaidia sana kurudisha imani ya nchi ambayo ukweli ipo ICU.
Mkuu, hapo utakuwa umeangalia upande mmoja. Tatizo la kifisadi linaloikumba nchi hii pamoja na matatizo mengine yanatokana na kukosa viongozi wenye hofu ya Mungu kwa imani yao.
Kauli za baadhi ya viongozi katika migogoro ya kidini baadhi ya sehemu kama Geita na kwingineko imetokana na viongozi kukosa weledi wa kiimani na ndio maana wanasiasa hukimbilia viongozi wa dini katika kutatua migogoro ya kidini.
Kwa hiyo, kuwa na viongozi wa kidini kushika nyadhifa mbalimbali za kisiasa ni point of advantage kwa wananchi kwani haki hutendeka! Kuna baadhi ya watumishi katika office za umma ninaowafamu, ni waumini wenye hofu ya Mungu (kwa imani zote) hakika akikuhudumia hutatamani kusikia mtu huyo kahamishwa idara.
Lakini wengine hao unawatetea wasiguswe na viongozi wa dini wao kuchomia matumbo yao tu, hawana lolote, Otherwise, labda ufunguke zaidi!