Katiba Mpya kama Sensa?

Katiba Mpya kama Sensa?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Tume ya Jaji Warioba imeshaanza kupokea maoni ya vyama vya siasa nchini juu ya nini hasa kiwepo na kiwepo kwa namna gani katika Katiba mpya.

Kwa mawazo yangu,naiona hatua hii kama ni hatua ya mwishomwisho kuelekea kuandikwa kwa Rasimu ya Katiba hiyo mpya.

Lakini,tupo wananchi tuliotamani kutoa maoni yetu lakini hatukufikiwa. Hivi,kukusanya maoni ndio kumeisha? Ndio yaleyale ya Sensa kwamba hata asiyefikiwa nyumbani kwake naye alihesabiwa?

Tusaidiane kujadili wana-JF
 
tuanzie hapa unaishi mkoa gani wilaya gani na kata ipi ikibidi weka na mtaa !
Maana kuna type ya watu walikuwa wanaamini wakusanya maoni watawafuata kwao.
 
tuanzie hapa unaishi mkoa gani wilaya gani na kata ipi ikibidi weka na mtaa !
Maana kuna type ya watu walikuwa wanaamini wakusanya maoni watawafuata kwao.

Dar es Salaam,Kinondoni,Mikocheni...Mikocheni B
 
Hata siku ya mwisho utashituka wakati Yesu ameshatutwaa tulio wake mawinguni.

Kila siku unachangia hapa JF, ulishindwaje basi hata kutuma maoni yako kwa njia ya mtandao.

Kweli kusoma sio kuelimika, endelea kusubiri ipo siku Judge Warioba atakufuata nyumbani kwako utoe maoni.
 
Back
Top Bottom