Katiba Mpya kuanzia kwenye vyama vya siasa, iwe ni awamu mbili tu kugombea tikeki ya uraisi

Maboso

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2013
Posts
5,164
Reaction score
5,762
Katika moja ya pitapita zangu kwenye social networks nimekutana na hii post ambayo kwa hakika imenikosha sana. Hiki alichokiongea huyu mdau kwa kiasi kikubwa kina ukweli ambao tulio wengi tumeufumbia macho.


Hapa chini ni michango ya followers wake

Anonymous 1
Economist anataka avunje record Na aingizwe kwenye kitabu cha maajabu ya dunia ...one of his dreams (nawaza)

Anonymous 2
Wanaongelea demokrasia lakn hatuon waktenda kwenye chama hvyo je wakpata urais nna mashaka sana ina maana hakuna mtu mweny cfa kwao je wakpata watatoa wap wa kusaidiana kuendesha nch dah huu wimbo mtamu sana acha niendelee kujiimbia mie

Anonymous 3

Anonymous 4
vyeti vyao vya kuzaliwa vya wenzio vimeandikwa hivyo vyeo, mpaka kifo sijui ndio kitawatenganisha au la.

Anonymous 5
kama mugabe tu, uchaguzi ni formality na hadaa ndani ya vyama vyao.

Anonymous 6
Nyakati zinakuja, watanzania waachane na ukiritimba... tunataka chama cha watanzania, sio chama na "Fulani", hii ni zaidi ya haki miliki

Anonymous 7
wa hao wanasiasa wetuinapofika kwenye fundo la wao kuwajibika, Basi neno demokrasia humaanisha 'mimi tuuu'

Anonymous 8

Anonymous 9
Wasomi c ndo hao wanaongelewa alaf wanaenda kuandamana badala ya kupma eti ksa kasema prof sasa cjui research walfanya za nn me napata tabu na wasomi wa dzain hyo cjui nan kairoga t.z yetu tumpe tuzo loh


 

Attachments

  • mdau-fb-net.jpg
    40 KB · Views: 272
Huu uzi unanipa shida sana kuuchangia maana kwenye Katiba Inayopendekezwa hakuna kipengele cha viongozi wa vyama vya siasa na Ukomo wao kukaa madarakani! Hivyo ni ngumu kwa kipengele hicho kuappear maana iko kwenye hatua za mwisho iende kupigiwa kura.

Suala la viongozi hao kukaa madarakani kwa muda mrefu ni la viongozi wenyewe na wanachama wao lakini lina ukakasi kweli maana toka mfumo wa vyama vingi kuanza kuna watu wamejigeuza miungu watu angalia orodha hii ya tangu kuanza kwa mfumo huo hapa Tanzania.

[COLOR=rgba(0, 0, 0, 0.701961)]

CHADEMA.
1992-1998. M/ kiti Edwin Mtei
1988-2003. M/kiti Bob Makani
2003-2008. Mkiti Freeman Mbowe
2009-2014. M/ kiti Freeman Mbowe
2014-2019. M/ kiti Freeman Mbowe


CCM ( Chama cha Mapinduzi)
1990-1996. M/ kiti Ali Hassan Mwinyi
1996-2006. M/ kiti Benjamin Mkapa
2006-2016. Mkiti Jakaya Kikwete


CUF (Civic United Front).
1995-2000. Mkiti Ibrahim Lipumba.
2000-2005. mkiti Ibrahimu Lipumba.
2005 -2011. mkiti Ibrahim Lipumba.
2011-2017 . mkiti Ibrahim Lipumba.


NCCR MAGEUZI.
1992-1995. Mkiti Mabere Marando.
1995-1999. Mkiti Augustin Mrema.
2000-2010. Mkiti James Mbatia.
2005-2010. Mkiti James Mbatia.
2010-2014. Mkiti James Mbatia.
2015-2020. Mkiti James Mbatia.




[/COLOR]​
 

Huo sasa ni ubabe! Hii sasa sifa!

Mtu huyu anayetamani kubaki kitini mpaka wamtusue atakuelewa unaposema demokrasia? Angalia hiyo orodha na mtiririko wake. Atapona huyo demokrasia? Kwao hii demo kwanza, rasia ni ya watu wengine siyo ya kwao. Ndiyo maana siku zote nasema "hawa ni madaraka oriented na wala siyo uzalendo. Kwa nini mtu huyo huyo tu? Mm! Shtuka
 

Mkuu ahsante sana kwa kuweka data muhimu kama hizi. Hakika mabadiliko yanatakiwa kuanza kuonekana kwenye vyama kabla ya kuingia kwenye uongozi wa nchi. Demokrasia ya kweli huanzia nyumbani.
 
Mkuu ahsante sana kwa kuweka data muhimu kama hizi. Hakika mabadiliko yanatakiwa kuanza kuonekana kwenye vyama kabla ya kuingia kwenye uongozi wa nchi. Demokrasia ya kweli huanzia nyumbani.

Hao ndiyo wachumia mdomo na kelele. Ukiona mtu anapiga kelele sana ujue kuna kitu anaficha. Hayo ndiyo mawazo ya wachumia tumbo wakati demokrasia yao ni ya mdomoni na siyo rohoni au moyoni
 
Upuuzi mtupu hakuna kitu hapo vilaza wote hao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…