tangu mjadala wa katiba mpya ulipo zinduliwa na rais ndani ya bunge,na kutopata baraka kutoka kwa wana ccm wenzake,hali imejidhihirisha hivi sasa baada ya bunge maalum la katiba kuanza vikao vyake,wajumbe wengi ambao zaidi ya 80% ni wana ccm wamejikita kwenye suala la posho baada ya kutafakari jinsi ya kutunga kanuni ambazo zitaboresha bunge la katiba,hili mijadala iwe mizuri na yenye tija kwa taifa.wao wamejikita zaidi kwenye kujadili kuwa posho ya laki 3 kwa siku haiwatoshi na wanashinikiza walipwe laki 7 kila siku,kama ilivyo tangazwa awali.kwa jinsi mambo yanavyo kwenda naona kuna kila dalili ya kuikosa katiba mpya yenye maoni ya wananchi.