KATIBA mpya kuipata itakuwa ndoto

sawa

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
2,752
Reaction score
929
tangu mjadala wa katiba mpya ulipo zinduliwa na rais ndani ya bunge,na kutopata baraka kutoka kwa wana ccm wenzake,hali imejidhihirisha hivi sasa baada ya bunge maalum la katiba kuanza vikao vyake,wajumbe wengi ambao zaidi ya 80% ni wana ccm wamejikita kwenye suala la posho baada ya kutafakari jinsi ya kutunga kanuni ambazo zitaboresha bunge la katiba,hili mijadala iwe mizuri na yenye tija kwa taifa.wao wamejikita zaidi kwenye kujadili kuwa posho ya laki 3 kwa siku haiwatoshi na wanashinikiza walipwe laki 7 kila siku,kama ilivyo tangazwa awali.kwa jinsi mambo yanavyo kwenda naona kuna kila dalili ya kuikosa katiba mpya yenye maoni ya wananchi.
 
rasmu mpya iitwe posho maana siku zaidi ya 3 zimepotea kwenye mjadala wa posho tu,kuwa laki3 kwa siku hazitoshi wanataka laki 7 hii nchi hii
 
Mh. Rais, na sisi wapiga kura wako, wananchi wa kawaida kabisa, walipa kodi na wanyonge wa nchi hii, kwa huruma zako tunakuomba nasi walau tupate hata 20000 kwa wiki maana hali yetu huku ni mbaya sana Mh. Rais.

Pia kati yetu tupo wenye uwezo wa kutunga katiba mpya kwa posho ya Tshs. 50000 kwa siku, kuliko hao wahuni ambao toka waende Dodoma hawawazi juu ya katiba mpya bali wameunga genge ovu kwa ajili ya kudai posho, inamaanisha kuwa nia yao na shauku yao ni pesa tu na sio katiba bora.

Mh. Rais nashangaa hadi sasa hao wahuni, watu wazima ambao yaonekana wamebalehe viungo vya uzazi tu na sio akili na bongo zao. Mimi ningekuwa ndie Rais ningetinga Dodoma na mmoja mmoja apite mbele ili aseme juu ya posho, ambaye anasema haitoshi angechapwa viboko na aende kwake akamuonyeshe mkewe/mmewe maana ya kuwa mzalendo, na yule ambaye yuko na mkewe huko, waliopelekana kihuni huko waonyeshane huko huko.

Natamani hilo bunge la katiba lingekuwa TARIME ili hao wasaghane na walisya wanaosema posho hazitoshi tuwaonyeshe nidhamu na uzalendo maana wangechapwa viboko na waende kulima mashamba ya vijiji. Muna Tata amanto ghayo ghaoyoka too.

NAOMBA WAHUSIKA MKITAKA KUJENGA BUNGE JIPYA MJENGE TARIME NA HUKO TUWASIKIE WANAOMBA POSHO KUBWA KUBWA. With
KWA HISANI YA ZZK fcbk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…