Katiba Mpya; kwanini CCM haina viongozi wenye weledi?

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
3,197
Reaction score
7,677
Mwenyekiti wa CCM, Samia alisema, katiba mpya isubiri kwanza. Angalao yeye hakusema kuwa katiba mpya siyo muhimu na wala hakusema siyo hitaji la wananchi.

Lakini ukimsikikiza Shaka na Chongolo, unajiukiza maswali mengi. Unajiuliza, ina maana ndani ya CCM yote, hawakupatikana watu wenye uelewa mpana, kumbukumbu ya uhakika na akili nzuri inayoweza kuwafanya waongee mambo kwa weledi, ili kuweza kuzishika hizo nafasi za juu za uongozi wa chama?

Chongolo na Shaka wamekuwa wapiga kelele badala ya kuwa viongozi katika kujenga hoja. Lakini ili ujenge hoja za kiweledi inatakiwa wewe mwenyewe uwe na weledi, na angalao IQ yako iwe above average.

Inashangaza sana, mtu kama Chongolo, katibu mkuu wa CCM, anasema eti katiba mpya siyo hitaji la wananchi!! Unajiuliza, hivi huyu ina maana hana uelewa, ni mwongo au ni mnafiki? Ina maana hajawahi kusoma ripoti ya Warioba kuhusiana na katiba mpya? Mwingine anasema eti katiba mpya ni hitaji la wanasiasa!! Unabaki unashangaa, sijui kama ni uduni wa uelewa au uwezo mdogo wa kufuatilia mambo.

Ripoti ya Warioba ilikuwa na mambo mengi sana. Ilieleza kwa kina ni nini wakulima wanataka kiwemo kwenye katiba mpya, wafanyabiashara wanataka katiba mpya iwe na kitu gani, wasomi walitaka kuwepo nini kwenye katiba mpya, wafanyakazi wanataka kuwe na nini ndani ya katiba mpya. Wanasiasa, wanataka katiba iseme nini kuhusiana na haki za kisiasa. Kulikuwa na maoni mengi ya makundi mbalimbali, na kulikuwa na maoni ya jumla kama vile kuhusiana na madaraka ya Rais na Mwungano.

Unapokuwa na viongozi wa chama ambao hawaelewi chochote kuhusiana na mambo haya, unashindwa kuelewa, ni nini hasa wanachokielewa. Au wanafikiri wameteuliwa kwaajili ya kuropoka na kupiga kelele?

Rais Samia hakuwahi kunena huu upuuzi wanaounena akina Chongolo na Shaka kwa sababu anaelewa fika kilichomo ndanibya repoti ya Warioba kuhusiana na maoni ya wananchi kutaka katiba mpya.

Huyu KM na Mwenezi wake, CCM wana kazi. Wameruka majivu, wamekanyaga makaa ya moto.
 
Ukiwa mwanasiasa ni lazima uwe mwongomwongo,mnafiki,wakujipendekeza?
 
MH mnaongelea katiba mpya! ni takwa la wanasiasa ni sahihi ni nani isiyeiishi siasa?
 
CCM wanajua katiba mpya itazaa tume huru ya uchaguzi na itakuwa mwisho wao
Kwa hiyo wanaamua kuacha yote muhimu yaliyopo kwenye rasimu ya Warioba, kwa sababu tu ya hofu ya kupoteza madaraka! Inashangaza sana na kuleta maswali mengi kama ndani ya CCM kuna watu wanaoipenda Tanzania.
 
Yani hii nchi wenye akili ni wanaoongozwa Ila viongozi chenga...leo atapiga nyungu hadharani kesho atadungwa sindano..Sasa ubabaki unajiuliza Kuna haja ipi ya kua na viongozi..uongozi ni msimamo na hekima
 
Kwa hiyo wanaamua kuacha yote muhimu yaliyopo kwenye rasimu ya Warioba, kwa sababu tu ya hofu ya kupoteza madaraka! Inashangaza sana na kuleta maswali mengi kama ndani ya CCM kuna watu wanaoipenda Tanzania.
Hakuna anayeipenda Tanzania zaidi ya watu kupenda familia zao
 
Mwenyekiti wa CCM, Samia alisema, katiba mpya isubiri kwanza. Angalao yeye hakusema kuwa katiba mpya siyo muhimu na wala hakusema siyo hitaji la wananchi.

Lakini ukimsikikiza Shaka na Chongolo, unajiukiza maswali mengi. Unajiuliza, ina maana ndani ya CCM yote, hawakupatikana watu wenye uelewa mpana, kumbukumbu ya uhakika na akili nzuri inayoweza kuwafanya waongee mambo kwa weledi, ili kuweza kuzishika hizo nafasi za juu za uongozi wa chama?

Chongolo na Shaka wamekuwa wapiga kelele badala ya kuwa viongozi katika kujenga hoja. Lakini ili ujenge hoja za kiweledi inatakiwa wewe mwenyewe uwe na weledi, na angalao IQ yako iwe above average.

Inashangaza sana, mtu kama Chongolo, katibu mkuu wa CCM, anasema eti katiba mpya siyo hitaji la wananchi!! Unajiuliza, hivi huyu ina maana hana uelewa, ni mwongo au ni mnafiki? Ina maana hajawahi kusoma ripoti ya Warioba kuhusiana na katiba mpya? Mwingine anasema eti katiba mpya ni hitaji la wanasiasa!! Unabaki unashangaa, sijui kama ni uduni wa uelewa au uwezo mdogo wa kufuatilia mambo.

Ripoti ya Warioba ilikuwa na mambo mengi sana. Ilieleza kwa kina ni nini wakulima wanataka kiwemo kwenye katiba mpya, wafanyabiashara wanataka katiba mpya iwe na kitu gani, wasomi walitaka kuwepo nini kwenye katiba mpya, wafanyakazi wanataka kuwe na nini ndani ya katiba mpya. Wanasiasa, wanataka katiba iseme nini kuhusiana na haki za kisiasa. Kulikuwa na maoni mengi ya makundi mbalimbali, na kulikuwa na maoni ya jumla kama vile kuhusiana na madaraka ya Rais na Mwungano.

Unapokuwa na viongozi wa chama ambao hawaelewi chochote kuhusiana na mambo haya, unashindwa kuelewa, ni nini hasa wanachokielewa. Au wanafikiri wameteuliwa kwaajili ya kuropoka na kupiga kelele?

Rais Samia hakuwahi kunena huu upuuzi wanaounena akina Chongolo na Shaka kwa sababu anaelewa fika kilichomo ndanibya repoti ya Warioba kuhusiana na maoni ya wananchi kutaka katiba mpya.

Huyu KM na Mwenezi wake, CCM wana kazi. Wameruka majivu, wamekanyaga makaa ya moto.
Wangekuwa na viongozi wenye weledi wasingetumia polisi kujibu hoja za wapinzani.
 
1CE22311-4A2C-4363-83A6-17D1B3F7FF57.jpeg
 
Back
Top Bottom