Katiba mpya: Mwenye uraia nchi mbili asigombee uongozi

Katiba mpya: Mwenye uraia nchi mbili asigombee uongozi

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2007
Posts
4,120
Reaction score
3,468
Nimekaa na kuwaza mambo mbali mbali kuhusu Mstakabali wa Nchi Yetu Tanzania. Nimetumia Three Phases: Tanzania Ilikotoka, Tnanzania Iliko sasa hivi, na Tanzania Ijayo.

Nimetafakari na kuyakumbuka mambo mengi mazuri sana ambayo Wagombea wa Urais walikuwa wakimwaga maneno matamu majukwaani kwa wananchi ili kuwashawishi wawapigie kura za ndio wapate nafasi zao.

Nyakati za J K Nyerere upigaji wa kura ulikuwa very LOGICAL. Kunakuwa na jedwali upande kuna picha ya J K Nyerere na chini ya picha yake kuna neno NDIYO kisha upande wa kulia kunakuwa na kivuli na chini ya kivuli kuna neno HAPANA.

Unapokuwa katika kiboksi cha kupigia kura katika hali kama hii hupati shida unaenda na kutia tiki katika kiboksi cha NDIYO kuashiria unamkubali J K Nyerere kuwa Rais wako. Kumbe LOGIC ni pale unapokuwa hutaki J K Nyerere awe Rais unachotakiwa ni kutia tiki kwenye kiboksi chenye kivuli chenye maandishi ya HAPANA. Maandishi haya HAPANA yalimkataa yeyote atakaye kaa badala ya kivuli na hivyo bado unamkubali J K Nyerere kuwa Rais.

Tulienda na Propaganda hizo hadi ikatakiwa kufanya MAZINGAOMBWE yaani KAMPENI. Katika Kampeni tumekuwa tukiahidiwa mambo mengi sana mazuri hadi imefikia ahadi zingine wahusika wenyewe wamesahau kama waliwahi kutoa ahadi kama hizo.

Mabadiliko ya mtindo wa AHADI na KAULI MBIU ni mambo makubwa sana ambayo ndiyo MAZINGAOMBWE YENYEWE. kama "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA" Lengo kubwa la kutoa ahadi hewa ni kufikia malengo waliyojiwekea kwa manufaa yao binafsi.

Maadili ya Uongozi kwa hawa wanaojiita Watawala badala ya kujiita Viongozi yamevunjwa na sasa viongozi wetu wamekuwa kama MCHWA katika kutafuna UHCUMI wa Taifa letu.
Kuna msemo unaosema "Mchwa huwa hawalali" Kama ndivyo!, ndugu zangu Tulale kwa zamu. Viongozi wetu WANATAFUNA NCHI KWA ZAMU HADI wamejilimbikizia mali nje ya nchi kiasi kwamba leo wanaogopa huenda wanaweza kufilisiwa mali zaoENDAPO HAWATAKUWA MADARAKANI na hivyo wanajipigia debe la kuhalalisha URAIA WA NCHI MBILI. URAIA WA NCHI MBILI NI KAMA kINYONGA, Hali ya mazingira humuwezesha kinyonga kubadilika kuweza kufanana na hali asilia. Kama itatokea hali ya mazingira ikabadilia ghafla kinyonga naye hubadilika hivyo hivyo. Ndivyo walivyo hawa. Vijana wengi baada ya kubanwa na hali ngumu ya maisha waliamua kujilipua kwenda ng'ambo wanaitwa akina "Ngapulila" Viongozi wetu hawa nao wanataka kuwa 'Modern Ngapulila" kwa kupitisha uraia wa nchi mbili.

Kwa ajili hiyo napendekeza kuwa katika Katiba Mpya Ijayo itamkwe wazi kwamba Mtanzania yeyote mwenye Uraia wa nchi mbili hataruhusiwa kugombea uongozi wowote wa Chama au Serikali nchini Tanzania. Pia itamkwe kwamba Kiongozi yeyote Mstaafu kama vile Rais, Mbunge, Diwani hadi ngazi ya chini kabisa aruhusiwe kuomba uraia wa nchi mbili miaka mitano baada ya kustaafu uongozi wake. Hii itasaidia kumchunguza yale aliyoyafanya wakati akiwa madarakani, pia kwa wale ambao watapenda kuwa na uraia wa nchi mbili watatakiwa kutafakari kwa kina kufanya hivyo kabla ya kuamua rasmi kuomba uraia huo wa kihindi.


Mungu Ibariki Afrika
Mungu Ibariki Tanzania
Nkosi Sekeleli Afrika
Nkosi Sekeleli Tanzania

Asanteni sana.
 
Laiti ungejua procedures za kuomba na kupata/kupewa uraia wa nchi nyingine sio suala la mtu kwakua alikua au ni kiongozi Tanzania basi atapewa uraia huo. Vigezo na masharti huzingatiwa na kutimiza masharti ni lazima.

Pili mdau mtoa mada fahamu sio kila anayechukua uraia wa nchi nyingine kajilipua na/au kutokana na Hali ngumu ya maisha kama unavyodhania ndio sababu ya kuchukua uraia wa nchi nyingine.

Tatu, kuwa na uraia wa nchi mbili haimfanyi kiongozi fisadi au mwenye makosa ya jinai nk kutopelekwa mahakamani sababu ya uraia wa nchi mbili. Hata ukiwa raia wa nchi moja ukifanya makosa katika nchi nyingine, sheria ya nchi husika ulipofanyia kosa hushika mkondo wake
 
Back
Top Bottom