Katiba mpya na mali za uma

Katiba mpya na mali za uma

msongamwanja

Member
Joined
Dec 30, 2013
Posts
20
Reaction score
2
Naomba wanajamii niwasilishe mada hakika kunamambo yananikera sana hadi hii leo lakini kwa waliopitia rasimu wanaweza nisaidia pia ktk hili
Tanzania inahitaji mabadiliko ktk kila nyanja hususani mtu au watendaji kutumia Mali za umma kama zao na wakiwa hawana wa kuwawajibisha ktk chili
Labda nianze na vyama vya siasa nini kusudio la kupewa ruzuku? Na kama Mm na uchache Wangu juu ya hili naweza kujibu ni kuvifanya hivi vyama viwe makini na kujiepusha na pesa chafu au kushindwa kujiendasha na kufanya siasa kuwa ya matabaka na kuzaaa chuki.
Sasa kama ndivyo kwa nn chama tawala bado kinahodhi na kushikilia miundombinu na vitegauchumi ambavyo ni zao la Tanganyika au Zanzibar yaani nazungumzia zama za TANU na ASP na hata baada ya CCM kuzaliwa 1977 kulikuwa hakuna utofautishaji kati ya mapato ya chama na ya taifa na wajumbe wa chama walilipwa na serikali.lakini ilipo fika mwaka 1993 Tanzania ilianza na kusaini makubaliano ya vyama vingi. Kama watendaji na viongozi wa zama hizo kwa kujua mihimili ya vyama vingi na umuhimu wake kwa nn hawakutenganisha na kuzibinafsisha Mali zote zilizomilikiwa na chama yaani CCM kuwa za Tanzania maana tunaenda ktk Tanzania mpya lakini chama kimoja na ni tawala kuhozi vyanzo vya mapato ambavyo ni jasho la kila mtanzania na c kila mwana CCM.
Ukitizama kwa undani utagundua takribani wizara zima ya michezo inahodhiwa na CCM yaani viwanja vyote vya mipira ni vyao kama Sheikh A. Abeid, CCM kirumba,Sokoine Mbeya, Sabasaba morogoro, dodoma,Tabora,Lindi,Mtwara na kwingineko lakin vile viwanja vyote vya wazi kutokana na Sera zao wamebadili matumizi kwa kujenga mashule au vimeuzwa kabisa
Sasa watanzania tunaenda kwenye katiba mpya tumejiandaaje pia kushuhudia wizara nzima ikiwa mikononi mwa upinzani? Tusiwe wepesi wa kusahau yaliyotokea zama waziri wa fedha ni Mh Mustapha Mkulo serikali ilipeleka muswada was kuvuta misamaha ya kodi ususani kwa taasisi za dini na baada ya hapo kulifuatiwa na vita baridi kati ya serikali na taasisi za dini kupelekea kupandishwa kwa ada za vyuo vya taasisi hizo sipendi Sema nani alishinda bali nataka kuwakumbusha tu.
Sasa ktk chili pia naomba tuwe makini nalo wanaforum na watanzania kwa ujumla haya ni mambo yetu na si mambo yao tukiwasusia wapange na watulishe ninashaka sana na haya
Naomba kuwakilisha hoja kwenu.
 
Back
Top Bottom