Nini kiliusumkuma Muungano kufanyika haraka, miezi 4 tu baada ya zanzibar kuwa huru? (April 1964).
NINI KIFANYIKE:
HATI YA MUUNGANO
MFANO:
- Jibu: Zanzibar baada ya kupata uhuru ilikuwa chini ya Sultani: Kwa sababu watu weusi walihisi bado wananyanyashwa ikabidi yafanyike mapinduzi ya Uongozi uliokuwepo (kama Misri/ Tunisia) Mapinduzi kuuondoa utawala uliopo madarakani kwa nguvu. Mapinduzi hayo ndiyo yalimfanya KARUME awe rais wa Zanzibar. Kama tunavyojua hakuna mapinduzi yoyote dunia yakawa salama, ni kwa sababu yule uliyempindua atajipanga upya kuja kukuondoa madarakani tena (Madaraka matamu). Njia pekee ya kuwa salama kwa serikali ya kimapinduzi ilikuwa ni lazima kuishi ndani ya KOTI LA NCHI YOYOTE YA JIRANI. NA NCHI ILIYOPATIKANA YENYE TAMADUNI ZINAZOFANANA ikawa TANGANYIKA. Hivyo kwa kumsaidia karume, mwl. Nyerere ikabidi waunganishe TANGANYIKA na ZANZIBAR na kuita TANZANIA- Manake ukisema unapigana/unaupindua uongozi wa serikali ya Zanzibar basi unakuwa umegusa TANZANIA NZIMA.
- Jibu: Tatizo ilikuwa usalama wa Zanzibar, suala la muungano ilikuwa maigizo; Ukiiguza Zanzibar ilikuwa lazima ukutane na Jeshi la JWTZ, Ukimpindua RAIS wa zanzibar unakuwa haujamaliza kwa sababu RAIS WA TANZANIA NAYE NI RAIS WA ZANZIBAR-Hivyo ulitakiwa umpindue na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania- Nani angeweza kufanya hivyo????????
NINI KIFANYIKE:
- Zanzibar iko salama kwa sasa, Tanganyika iko salama; Tatizo lililopo ni SIASA; Wanasiasa wanaogopa endapo IKIWA SERIKALI TATU; wale wanaofaidika na serikali mbili itakula kwao, Vile vile chama kinachokubalika upande mmoja wa nchi kinaweza kupata shida kuongoza katika mfumo huo. IKIWA SERIKALI MOJA; Hapa ndipo wa ZANZIBAR HAWATAKI, wao waliutumia muungano kama kulinda Mapinduzi na si kuungana moja kwa moja, kuliko serikali MOJA watasema bora kila mtu asepe kivyake. IKIWA SERIKALI MBILI: Hii wanataka wale wanaonufaika na muungano sasa waendelee kunufaika, japo hili linaweza kuwa bomu kwao siku za usoni.
HATI YA MUUNGANO
- Sina hakika ila niliwahi kusikia kuwa hati ya muungano haipo; Haipo kwa sababu ilikuwa makubaliano ya watu wawili mmoja (nyerere) akitaka kuimarisha ulinzi wa mwenzake ili asipinduliwe (karume).
MFANO:
- Baada ya Ghadaf Kupinduliwa, kama Libya ingeamua kuungana na nchi yoyote ya jirani (Hata kimaigizo) Machafuko haya tunayoyaona yasingetokea tena.
- Kuna watu waliomba uhamisho: Wakafoji vyeti vya ndoa kwa muda ili baada ya uhamisho tu, kila mtu kivyake-Kilichotokea, baada ya Uhamisho Mwanamke akang'ang'ania kuwa Umenioa kihalali na CHETI cha ndoa ninacho; HICHO NDICHO KINACHOTOKEA KWENYE MUUNGANO WETU.