dudus
JF-Expert Member
- Feb 28, 2011
- 23,782
- 54,213
Umofia kwenu wanajamvi.
Natumaini wote mmesikia nguli wawili wa siasa za Afrika Dr. Robert Gabriel Mugabe na General Yoweri Kaguta Museveni wakiilaani vikali dunia ya magharibi kwa kutaka kulazimisha ushoga (homosexuality) Afrika kama sharti au kigezo kimojawapo cha "demokrasia". Kwanza niwapongeze marais wetu hawa bila kumsahau Goodluck Jonathan wa Nigeria ambaye tayari alishasaini sheria ya kukataa ushoga nchini mwake. Nalaani kwa nguvu zote (japo ni mambo ya ndani ya nchi zao) hatua ya mataifa mawili Afrika kututia aibu waafrika - Afrika Kusini na Malawi kwa kukubali ushoga ndani ya mataifa yao.
Sasa basi:-
(i) kwa kuwa tuko kwenye hatua muhimu zaidi ya kuandika Katiba Mpya ambayo ni sheria mama na tayari wajumbe wa kutimiza wajibu huu mkuu na uliotukuka wako Dodoma kwa kazi hii adhimu;
(ii) na kwa kuwa kwa hulka ya viongozi wetu ya "kuonea aibu wazungu" ipo hatari ya kukubali masharti ya ajabu ajabu kama ushoga kwa ndoano ya misaada;
Ni ombi au pendekezo langu kwenu wanajamvi tuwaombe Waheshimiwa Wabunge wa Bunge Maalumu kuingiza kipengele cha kukataa ushoga katika Katiba Mpya. Kwa kufanya hivi, sheria, azimio, au jambo lolote lenye mwelekeo wa kishoga automatically litakuwa batili. Kiongozi yeyote au taasisi yoyote (chama cha siasa, taasisi za kidini, n.k.) zitakazo-support vitendo vya kishoga iwe kwa uwazi au kwa taathira yake vibatilishwe ndani ya ardhi ya Tanzania haraka iwezekanavyo. Ni kwa kufanya hivi tutalinda tunu za taifa letu, tutalinda vizazi vyetu, na tutalinda taifa letu.
Ndoa (na mahusiano ya kingono) ni lazima itokane na jinsi mbili tofauti na sio vinginevyo. SAY NO TO HOMOSEXUALITY NOW!