Katiba mpya na uvivu wetu wa kufikiri

Katiba mpya na uvivu wetu wa kufikiri

kasema

Member
Joined
Sep 27, 2010
Posts
22
Reaction score
9
Watu tumekuwa busy na katiba mpya,hilo ni zuri sana lakini tumekuwa busy na kipengere saana kimoja cha muungano na nahisi hata warioba nae akili yake iko busy kutoka siku anateuliwa mpaka leo busy na jambo la muungano kwamba tuwe na serikali 3.

Ukitazama vyama vingine vya siasa kama chadema wao wako busy na muungano kwa maana ya serikali 3 na kusahau kuwa wao bungeni walikuwa wakipigania eti serikali ya ccm ina serikali kuubwa ambayo inameza fedha za umma.,yaani Other charges kubwa Develoomemt expenditure inkuwa ndogo....

Chadema wamesahau hilo.....lakini nadhan kwa maslah binafsi kwani navyofikiri mimi serikali 3 ndo itakuwa mchwa wa fedha za umma.

Ccm na wao eti wako busy na serikali 2 hawatoi misimamo mingine ktk kuwatetea watanzania ktk kupata katibu mutribu??????

Asasi za kiraia am sure zitakuwa busy na manbo ya jinsia,usawa na usishangae wakataka hata mashoga watambuliwe.....

Wooote wamesahau kama nchi kuongozwa lazima iwe na fedha....hawazungumziii ni namna gani katiba itaitaka au itasema jini juu ya kukusanya kodi ili kuwapatia watanzania maendeleo....ila imesema ni jinsi gani serikali itatumia fedha...huuu ni upuuuz maana yake ni kwamba unapata mtoto kabla hata huja sex na mkeo,je huyo bado utamuita mkeo???


Tuamke na wajumbe la katiba wataamka.....nadhan jambo la msingi kabisa ni kukusanya kodi na katiba iseme wazi tusisubiri regulations zitatumaliza na kodi kubwa zisiende kwa watumishi bali migodi na kuondoa misamaha isiyo na tija.
 
Wewe ndo unashangaza , sikutegemea uandike haya uliyo yaandika hivi kweli katiba ndio inapaswa ieleze kodi zitakusanywaje ? majabu kweli ! hivi mpaka leo ujajua kuwa kuna sheria mbalimbali zinazosimamia uendeshaji wa serikali ikiwemo na hilo la kodi ambapo zipo sheria chini ya TRA, tatizo la Tanzania liko kwenye uongozi, hatuna kiongozi makini aliyewahi kutokea kusimamia utawala wa sheria
 
Labda nikuulize swali jepesi kabla hujafikiria beyond your scope. Nini maana ya katiba? Maana naona kama kuna mkanganyo wa mambo kwenye analysis yako!
 
Wewe ndo unashangaza , sikutegemea uandike haya uliyo yaandika hivi kweli katiba ndio inapaswa ieleze kodi zitakusanywaje ? majabu kweli ! hivi mpaka leo ujajua kuwa kuna sheria mbalimbali zinazosimamia uendeshaji wa serikali ikiwemo na hilo la kodi ambapo zipo sheria chini ya TRA, tatizo la Tanzania liko kwenye uongozi, hatuna kiongozi makini aliyewahi kutokea kusimamia utawala wa sheria

Katiba ni sheria mama na kama sheria mama haitasema chochote kuhusu mapato ya nchi hakuna tutakapokwenda kwasababu baadae regulations zitakazokuja zitaishia kuwa na mianya ya wizi...mfano mdogo ni katika katiba iliyopo haitilii mkazo namna bora ya kukusanya kodi na kuzikinda dhidi ya mafisadi na wezi leo useme uachie serikali kutunga regulations unadhan tutapona???
 
Back
Top Bottom