Sir robby
JF-Expert Member
- Jun 22, 2022
- 2,396
- 4,080
Wadau nawasalimu,
Katiba Mpya ni kilio cha Watanzania kwa hivi sasa. Tatizo la katiba iliyopo ni la muda mrefu sana, karibia miaka 60 ya Uhuru. Nchi imekuwa na Marais 6 kwa sasa, hakuna Rais aliyeibadilisha Katiba iliyopo, katiba ambayo iliyotungwa bila kuwashirikisha wananchi ni Katiba ya viongozi.
Wakati wa utawala wa Awamu ya 4 Rais Kikwete aliamua kuwapatia Watanzania Katiba Mpya na wananchi walishiriki kutoa maoni na mapendekezo yao lakini hakufanikiwa kutokana na mahafidhina wa chama chake kutokuta mabadiliko na kupelekea mchakato wa Katiba Mpya kufa.
Alipoingia Rais Magufuli yeye bila aibu hakutaka kabisa kusikia suala la Katiba mpya kwani Katiba iliyopo inawapa madaraka makubwa sana viongozi wetu ndio sababu ya kutokutaka mabadiliko ya Katiba Mpya.
Kutokana na Marais wa 5 waliopita kushindwa kabisa kuwapatia wananchi Katiba Mpya namshauri Rais Samia awapatie Watanzania Katiba Mpya kwa kuwashirikisha katika kuitunga kutoa maoni na mapendekezo hakika atakuwa kajitengenezea "Legacy isiyosahaulika" atakumbukwa kama shujaa wa Katiba Mpya katiba iliyowashinda watangulizi wake.
Kiu ya Watanzania ni kuona nchi yao inafanya mabadiliko ya Katiba ili iendane na mabadiliko ya mambo mengi.