sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,687
- 1,111
Toka tupate uhuru ni miaka sasa zaidi ya 55,kama nchi tumepitia mabadiliko mbalimbali ya mchakato wa katiba ya Jamhuri ya Muungano,hatujawahi kupata katiba iliyotokana na matakwa ya wananchi.
Pamoja na matukio mbalimbali yaliyosababisha kufanyiwa marekebisho, kwa awamu mbali, kama kipindi tulipo ungana Bara na Visiwani,ilitulazimu kuingizwa ingizo jipya linalohusu mambo ya Muungano.
Likaja suala la haki za binadamu mara baada ya kusaini mkataba wa amani, pia mfumo wa vyama vingi. Lakini pamoja na maingizo haya mapya bado tuna uhitaji wa katiba ya wananchi,iliyoshirikisha na kukusanya maoni ya Watanzania.
Kwa nia njema kabisa bila kuzingatia ilani ya chama chake, aliyekuwa Rais wa awamu ya nne, alianzisha mchakato wa katiba ya wananchi kwa kuunda tume iliyoratibu maoni ya wananchi chini ya M/kiti Jaji Warioba, ambaye baada ya shughuli kubwa waliandaa rasimu ya katiba iliyowakilishwa kwenye Bunge la katiba.
Mchakato huu uligharimu fedha za walipa kodi zaidi ya shilingi bilioni 300,lakini mchakato uliharibiwa na itikadi za kichama, hali iliyopelekea Bunge la katiba kupuuza maoni ya wananchi chini ya Jaji Warioba na kuingiza maoni ya chama cha Mapinduzi. Hali iliyopelekea kuzua mtafaruku mkubwa baina ya pande mbili na kuzaliwa kwa kundi la UKAWA.
Yapo mengi yaliyohodhiwa na M/Kiti wa bunge la Katiba, ikiwa ni pamoja na kuvunja sheria na kanuni, ili kupitisha wayatakayo wao si wananchi.
Tuachane na hayo, turudi kwenye hoja kwanini iwe sasa. Itakumbukuwa kuwa mbali na figisu za win win situation, mchakato wa kuandika rasimu iliyokusanya maoni ya wananch ilikuwa tayari na kwa kuwa kazi kubwa ilikwisha fanyika kwanini sasa kazi ya kuipitisha isifanyike, kwa kiss kutokana na hali ya sasa hitaji la katiba ni kubwa kuliko maneno ya watawala wanaobeza kuwa katiba mpya si muarobaini wa matatizo ya wananchi hatuna budi kuitaka serikali kulirudisha kwenye Bunge la katiba ili kumalizia kazi iliyobaki
Hitaji la katiba mpya kwa sasa ni kubwa kuliko wakati mwingine wowote, kutokana na mabadiliko ya kimfumo na mahitaji ya Watanzania wa sasa.
Msingi wa katiba ya 1977 lilikuwa ni takwa la kikundi cha watu wachache, waliohodhi mamlaka na madaraka kwa kipindi kile,ambao kwa katiba hiyo ilitengeneza utawala wa kifalme wenye kulinda na kuminya ugatuaji madaraka kwa wananchi.
Ndiyo maana kwa katiba hii ya 1977 hakuna mtawala mpenda madaraka atayekubali kuibadilisha,kwa kuwa kuibadilisha ni kutoa nafasi ya kuwapa wananchi nguvu ya kumuondolea mtawala madaraka makubwa aliyo nayo.
Kwa katiba hii, mtawala akikanyaga katiba hakuna mamlaka yenye kuhoji isipokuwa tu mwananchi huyu amepewa mamlaka katika haki ya kupiga kura tu, wakishapiga hawana haki ya kuhoji matokeo ya urais popote pale, hali inayomjengea mtawala kiburi cha madaraka.
Ndiyo maana Mwalimu Nyerere aliwahi kuonya pamoja na kuwa ndiyo waliyoitunga katiba ya 1977 kuwa,kwa katiba hii ikipata mtu kichaa inamfanya kuwa dikitekta,sisi kama taifa hatuhitaji hali hiyo.
Ukiangalia kwa kina utaona kuwa yapo mambo mengi ambayo hayahitaji kuwa ingizo jipya,yaani kiraka kipya zaidi ya kudai katiba mpya ya wananchi, itakanayo na matakwa ya wananchi, ambayo yapo kwenye rasimu ya katiba iliyosimamiwa na Jaji Warioba.
Tumeona watawala wanabeza na kusema katiba mpya si muarobaini wa matatizo ya watanzania,tuambieni muarobaini wa matatizo ya watanzania ni upi,kwanini tuliwaingiza chaka Watanzania kwa mchakato usio suluhisho la matatizo ya wananchi!!!
Watawala wanafikiri takwa la katiba ni suala la hisani ya mtawala, katiba haiombwi kama kipande cha mkate,ni haki na hitaji halali la wananchi hata Kama litadhoofisha nguvu ya mamlaka ya watawala. Tunataka katiba inayotoa haki kwa mikono yote miwili si,mkono wa kulia unatoa haki, mkono wa kushoto unanyang'anya.
Kwa kuwa kodi ni mali yetu, na katiba ni hitaji letu hatuna budi kuidai katiba ambayo itatoa mwongozo kwa mambo mbalimbali,bila kuzingatia utashi wa mtawala.
Mathalani leo rais anasimamia miradi mikubwa inayogharimu fedha zetu za kodi, hajui kama uchaguzi ujao atakuwa tena rais, kwa katiba hii atayekuja naye atakuja na mambo yake ambayo anaweza kusema si kipau mbele chake miradi aliyeikuta haijaisha, tukajikuta miradi ina kwama na pesa zetu zinapotea bure.
Tunataka uwazi wa mikataba isiwe ya siri kama vikao vya unyago, usiri huu ndiyo chocheo la rushwa kwa watawala hali inayoisababishia nchi hasara kubwa.
Kwa Mtanzania mwenye upendo na nchi yake, asiione katiba ni adui wa mambo yake, tukimjua tutamkataa bila kujali rangi ya sura yake. Tunataka Katiba mpya itakayo ondoa michezo ya watu wenye kuichezea katiba kwa maslahi yao,huku wakikanyaga katiba hiyo kwa kupora haki za binadamu.
#Hitajiletukatibampya#