Katiba Mpya - Ndoa ya Wanaume Wengi kwa Mwananke Mmoja iwe Ruksa

Katiba Mpya - Ndoa ya Wanaume Wengi kwa Mwananke Mmoja iwe Ruksa

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Kwa vile imezoeleka kuwa wanaume ndiyo wenye mamlaka ya mwisho katika mahusiano ya ndoa - kuoa zaidi ya mwanamke mmoja (ambao ni mfumo dume)
"Natumaini sasa imefika wakati wanawake nao, wakubaliwe kuolewa na wanaume wengi wakati wakiendeleza mahusiano ya kifamilia. Na wapewe uwezo na mamlaka ya kutoa talaka"

...natumaini wanawake wakiwezeshwa inawezekana...

Soma NUKUU hapo chini:

"Wanaume wawili wa Kenya wamesaini makubaliano ya kumuoa mwanamke mmoja. Mwanamke huyo alikuwa na uhusiano kwa wakati mmoja na wanaume hao kwa miaka minne na amekataa kumchagua mmoja.
Makubaliano hayo yanawaruhusu wanaume hao, Sylvester Mwendwa na Elijah Kimani kuishi na mwanamke huyo nyumbani kwake na watamsaidia kuwalea watoto wawili alionao. Gazeti la Daily Nation limeandika kuwa Mwendwa na Kimani wamelazimika kukubaliana hivyo baada ya kubaini kuwa wote walikuwa na uhusiano na mwanamke huyo wa Mombasa.
Sehemu ya makubaliano hayo inasema: Mimi Sylvester Mwendwa na Bw Elija Kimani, tume- kubaliana yakuwa kuanzia leo hatutawahi kubishana wala kuoneana wivu kwa ajili tayari tumejuana na mke ambaye anaitwa Joyce Wamboi ambaye amesema hayuko tayari kupotezapenzi letu.¡±
¡°Kila mmoja ataheshimu siku aliyopangiwa. Tunakubaliana kupendana na kuishi kwa amani. Hakuna aliyetulazimisha kufikia makubaliano haya.¡±
Mwenda amesema wazazi wake wamempa baraka zote na sasa anajiandaa kutoa mahari. Mwanamke huyo ni mjane na anawatoto wawili.

Source: Daily Nation, NTV, BBC,
 
Back
Top Bottom