Katiba mpya ni muhimu leo, sio kesho

Katiba mpya ni muhimu leo, sio kesho

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kwa unyenyekevu mkubwa Rais Samia ashauriwe ili nae apange kalenda ya mchakato wa kumalizia uwandishi wa katiba mpya. Sio rahisi kwa mwaka huu kuandika katiba mpya kwakuwa bajeti ya mwaka huu haina kifungu cha uwandishi wa katiba mpya.

Lakini sio vibaya Mama yetu akasema kazi ya kukamikisha katiba mpya itaanza lini pamoja kwamba tunakabiliwa na umaliziaji wa miradi yetu mikubwa ya Reli, Bwawa, upatikanaji wa maji na umeme vijijini ambayo ni miradi muhimu sana.

Katiba mpya ni muhimu sawa na maisha ya mtu kwakuwa katiba hii ya Sasa inategemea sana uadilifu na utashi wa kiongozi aliyeko madarakani. Mama yetu ni muadilidifu sana asiye na mashaka LAKINI hatujui baada ya mama Samia atakuja nani kwa njia gani lini. Hofu ya aina hii wanayo watu wengi hata wanaomzunguuka Rais.

Katiba mpya ni yetu sote na Ina manufaa kwetu sote kama taifa. Hivyo, upatikaji wake usitugombanishe na kututenga Kati ya watawala na wapinzani. Huu ni mustakali wetu.
 
Tunavigezo gani kupima uadilifu wake? Je, matamko tu hutosha? Nani kafanya upembuzi kujua yaliyomo katika utawala wake ndani ya siku chache?

Hoja ya umuhimu wa katiba, nakuunga mkono.

Sent from my SM-J701F using JamiiForums mobile app
 
Tunavigezo gani kupima uadilifu wake? Je, matamko tu hutosha? Nani kafanya upembuzi kujua yaliyomo katika utawala wake ndani ya siku chache?

Hoja ya umuhimu wa katiba, nakuunga mkono.

Sent from my SM-J701F using JamiiForums mobile app
Nadhani ni mwadilifu kwa kutumia vigezo vifuatavyo:

Kuna harufu ya utawala wa sheria inasikika kwa mbali, ingawa ni bado mapema:
1. Sijasikia mtu amepotea
2. sijasikia mtu katumbuliwa kwenye mkutano hadharani.
3. Anadhamini wanaoidai serikali na kuwalipa madeni yao
4. Amekiri kuwa corona ipo, chukueni hatua
5. Amerekebisha mahusiano na majirani zetu ambayo yalipotea
6. Ni msikivu, kasikia kilio cha miamala fasta. Washauri walimshauri vibaya, awapige jicho ajue dhamira yao.
7. Sioni magari ya askari yakivunja sheria za barabarani ovyo, yakijifanya yako kwenye dharura all the time.
8. Mama hajavaa nguo za kijeshi bado mpaka sasa, na hatujui kama kuna siku nae atazijaribu.
9. Matumizi ya wanaharakati wa kujitegemea wanaotukana watu hakuna.
10. mitandaoni tunaandika kidemokrasia kabisa, mama anasoma tu na yeye na kuishia kutikisa kichwa kama wengine.

Matukio yaliyolikuta taifa kwenye awamu ya Tano yameliunganisha taifa kujua udhaifu wa katiba ya sasa na umuhimu wa kuwa na katiba mpya.
 
Back
Top Bottom