Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,899
- 10,415
Katiba mpya ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa hata chama bila katiba hakiwezi kuendelea.
Katiba ya sasa ina mapungufu mengi sana. Kwanza swala la elimu halikuzingatiwa kabisa katika kuwapata viongozi mbalimbali.
Dunia ya sasa inaongozwa na sayansi na teknolojia. Huwezi kushindana katika ulimwengu unaotumia sayansi na teknolojia bila kutumia watu walioelimika kwa kukaa darasani. Hata kama watanzania wengi waliopata elimu hawaleti matokeo mazuri kwenye taifa hilo limetokana na kuwatumia viongozi wasio na elimu kwenye taifa letu.
KATIBA ndio dira ya maendeleo kwenye chama chochote. Ndio kiongozi. Sasa kama katiba ndio dira ya maendeleo kwa Chama itakuwaje kwa taifa.
Maendeleo yatakuja kwa kasi sana.
Tukiwa na vitu vifuatavyo.
TUME HURU, hapa viongozi huwa wanajisahau sana wakidhani nchi ni yao peke yao, majimbo ni yao peke yao. Maendeleo jimboni hayaonekani watu wanakula tu mishahara ya serikali. Sasa tukiwa na tume huru itakua ni rahisi kuwaondoa viongozi wazembe ambao hawafanyi vizuri.
Separation of power kwenye mihimili ya serikali. Hapa ni pa muhimu mnooo
Swala la elimu, uzoefu, knowledge na ujuzi lizingatiwe kwenye kuteua na kuchagua viongozi
Itapendeza ikiwa hivi.
1. Mwenyekiti na mtendaji wa kijiji awe elimu ya certificate na kuendelea.
2. Diwani, awe na elimu ya diploma na kuendelea.
2. Mbunge, awe na elimu ya Degree na kuendelea.
3. Mbunge asiwe waziri, waziri asiteuliwe atume nafasi ya maombi ya kazi. Na awe na elimu ya wizara anayoomba kazi.
N.k.. n.k.
Viongozi wa kuokoteza wasio na elimu tuwatupilie mbali kwenye katiba, elimu ipewe kipaumbele kwenye katiba. Hapo ndipo hata viongozi wataipa elimu kipa umbele.
Elimu iwe dira ya maendeleo na sio ujanja ujanja wa kubahatisha. Nchi iongozwe kwa tafiti za kisayansi na sio ujanja ujanja wa kubahatisha. Sayansi na teknolojia na tafiti vipewe kipaumbele katika taifa.