Katiba Mpya ni watu, Marafiki wala Maadui hawawezi kuwa wa Kudumu

Katiba Mpya ni watu, Marafiki wala Maadui hawawezi kuwa wa Kudumu

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Ni dhahiri kuwa NCCR, CUF, Chadema na wengine pia wapo wanahitaji katiba mpya sasa.

Katiba mpya itakuwa mustakabala wetu ulio bora zaidi kama nchi. Hayupo mwenye akili timamu anayeweza kuupinga mchakato wake.

IMG_20220405_112819_728.jpg

Tunaotaka mustakabala mpya tupo chini ya meza. Wasiotaka mustakabala mpya wako juu ya meza, wanatumbua!

Chini ya meza ni jukumu letu kufahamiana. Tunahitajika kusimama kwa pamoja tu, ili kuweza kujikomboa.

Wanahitajika wanaoweza kuwa tayari kusimama bila kujali waliwahi kuwa marafiki au maadui.

Asiyekuwa tayari kusimama sasa, hata kama ni rafiki, hatufai huyo.

Aliye tayari kusimama sasa hata kama ni adui, huyo anatufaa.

Kwa sasa cha muhimu zaidi kuliko vyote ni kufahamiana na mashirikiano ya aina yoyote kuelekea kusimama.

Shime waungwana. Umoja ni nguvu.
 
Watanzania wengi wameichoka CCM kupita maelezo, Lissu ana ushawishi mkubwa sana kwa raia wengi. Ogopa mtu asiyetumia pesa wala asiye na madaraka lakini anaaminiwa na wengi kama tumaini lao la kuwatoa katika hali waliyo nayo.
ASANTE SKY! upo?
 
Siyo siri Lissu na Mbowe wanakubalika na wanao uwezo wa kutuunganisha kusimama chini ya meza.

Tunavyovitaka sasa ni kufahamiana kuelekea kusimama chini ya meza bila kujali vyama.

IMG_20220405_124518_576.jpg

Ndani ya vyama kuna waoga kama ambavyo majasiri wapo.

Kipaumbele iwe ni kusimama chini ya meza.
 
"Aliye tayari kusimama sasa hata kama ni adui huyo anatufaa"

Hapo sawa, ila isitokee aliye nyuma aanze kutafutwa na kubembelezwa ili aje ajiunge na wengine, kwa kufanya hivyo tutakuwa tunapotezeana muda na kuichelewesha zaidi Katiba Mpya.
 
Hatuko kwenye kubembelezana. Tuko kwenye kuchukua hatua. Sana sana ni kufahamiana tu.

Ikumbukwe:

Wanufaika wa Katiba Iliyopo hawahitaji elimu
 
Back
Top Bottom