Katiba mpya ni ya vyama au wananchi?

Katiba mpya ni ya vyama au wananchi?

Andongwisye

Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
30
Reaction score
5
Hivi misimamo ya CCM na Chadema kwenye mchakato wa katiba ni halali? siongelei usiriki ninachoongelea ni kampeni za kuwaelekeza wananchi nini cha kufanya na nini kinatakiwa kwa mtindo huu tutapata katiba mpya?
 
Mkuu, vyama pia ni vya wananchi.Nadhani jambo la muhimu ni wanachokijadili kina maslahi kwa taifa?
 
Hivi misimamo ya CCM na Chadema kwenye mchakato wa katiba ni halali? siongelei usiriki ninachoongelea ni kampeni za kuwaelekeza wananchi nini cha kufanya na nini kinatakiwa kwa mtindo huu tutapata katiba mpya?
Ni halali. Kila mahali panapotokea kuandika katiba mpya huwa inakuwa hivyo. Kule Kenya walikuwawanaita CHUNGWA na NDIZI. Wengine katika rasimu ya Katiba yao walikuwa mrengo wa chungwa na wengine mrengo wa ndizi. Kwao ilikuwa kampeni kubwa sana. Hii hapa ni kitu kama kidhaifudhaifu hivi. Kule ilikuwa kwenye vituo vya mabasi masokoni na kila penye mikusanyiko ya watu. Kwenye matatu (daladala) watu wanakuuliza kuwa wewe ni chungwa au ni ndizi. Mwishonii walipopiga kura na ukawa mwisho wa kampeni. Hapa bado kabisa.Unajua WaTZ kawaida ni waoga.
 
Katiba Mpya ikiwezesha kuhamia Dodoma itakuwa katiba Bora kuliko zote kwani itakuwa imetekeleza ahadi ambayo imekuwa ngumu kutekelezeka kwa Miaka kibao japo CDA wapo wametulia .
 
Mshunami nakubaliana na wewe ila kwenye uoga hatuna uoga ila tunapandikizwa uoga. Labda tujiulize kama ni uoga tunaogopa nini? Labda kwenye vurugu kweli sisi ni waoga kufanya vurugu nami ni muoga katika hilo. Kenya ilikua maslahi ya nchi na hakukua na mtu anayezungumzia wale waliotaka kujitenga wa Mombasa la hasha wala hakuna mtu aliyewaambia wakenya wachague ndizi au chungwa wakati wa maoni bali waliambiwa hivyo/ kampeni zilifanywa wakati wa referendum yaani wakati wa kupiga kura.

Anachouliza mtoa mada ni kwamba kwanini viongozi wa vyama ndiyo wanawaelekeza wananchi watoe maoni fulani wasitoe maoni fulani? kwanini viongozi wa kidini wanawaambia wananchi watoe maoni fulani waache fulani? anachoona mtoa mada nami namsapoti ni kuwa vyama fulani hasa kimoja kinachotumia hela za wafadhili kuwahadaa wananchi kama ilivyo kwa Kibamba anavyojaribu kulazimisha katiba iwe kama anavyotaka yeye bila kutueleza udikteta aoufanya pale ofisini kwake kwa kulazimisha mawazo yake ndiyo ya heshimiwe ya wengine hayana maana.

Tubadilike tuache ulimbukeni wa kisiasa.
 
Back
Top Bottom