Mshunami nakubaliana na wewe ila kwenye uoga hatuna uoga ila tunapandikizwa uoga. Labda tujiulize kama ni uoga tunaogopa nini? Labda kwenye vurugu kweli sisi ni waoga kufanya vurugu nami ni muoga katika hilo. Kenya ilikua maslahi ya nchi na hakukua na mtu anayezungumzia wale waliotaka kujitenga wa Mombasa la hasha wala hakuna mtu aliyewaambia wakenya wachague ndizi au chungwa wakati wa maoni bali waliambiwa hivyo/ kampeni zilifanywa wakati wa referendum yaani wakati wa kupiga kura.
Anachouliza mtoa mada ni kwamba kwanini viongozi wa vyama ndiyo wanawaelekeza wananchi watoe maoni fulani wasitoe maoni fulani? kwanini viongozi wa kidini wanawaambia wananchi watoe maoni fulani waache fulani? anachoona mtoa mada nami namsapoti ni kuwa vyama fulani hasa kimoja kinachotumia hela za wafadhili kuwahadaa wananchi kama ilivyo kwa Kibamba anavyojaribu kulazimisha katiba iwe kama anavyotaka yeye bila kutueleza udikteta aoufanya pale ofisini kwake kwa kulazimisha mawazo yake ndiyo ya heshimiwe ya wengine hayana maana.
Tubadilike tuache ulimbukeni wa kisiasa.