Kwa kuwa tume nyingi za wazawa ziliundwa na kutoa maoni/mapendekezo ya kuwa na serikali tatu lakini wanene ndani ya CCM hawataki, nimeona kumbe mheshimiwa Rais angeteuwa watu toka nje kuunda tume ya rasimu ya katiba mpya. Hii ingekuwa kama dawa ya kutibu ukusanyaji wa madeni ya TANESCO uliofanywa na serikali ya awamu ya tatu. Kwa kuteuwa watu wa nje nina hakika baadhi ya wanene ndani ya CCM wataufyata tu na wananchi wakapata wanachokihitaji katika katiba mpya ya nchi yetu.