palalisote
JF-Expert Member
- Aug 4, 2010
- 8,335
- 1,459
KAMA Watanzania wataridhia rasimu ya katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyozinduliwa wiki iliyopita na Tume ya Mabadiliko ya Katiba bila mabadiliko, itapiga marufuku Rais wa Tanzania kujihusisha kwa namna yoyote na chama chochote cha siasa kikiwemo chama chake.
Pendekezo hilo limo katika Ibara ya 69 ya rasimu hiyo inayobainisha madaraka na majukumu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.
Ibara ya 69(4) ya rasimu hiyo inabainisha kuwa: Katika kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa ibara hii, rais ataepuka kujinasibisha, kwa namna yoyote ile, na chama chochote cha siasa au kundi lolote kwa namna ambayo inaathiri umoja wa wananchi.
Katika ibara inayotangulia, ya 68(2) Rais wa Jamhuri ya Muungano ametajwa kuwa atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu, na kwa mamlaka hayo kwanza atakuwa alama na taswira ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na watu wake, pili atakuwa alama ya umoja na uhuru wa nchi na mamlaka yake na mwisho atakuwa na dhamana ya kukuza na kuhifadhi umoja wa kitaifa.
Lengo la kuwekwa marufuku hiyo limebainishwa wazi na ibara yenyewe kuwa ni kulinda umoja wa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na umoja wa kitaifa kwa ujumla.
Kama rasimu hiyo itapitishwa katika kura ya maoni mwakani, rais hataruhusiwa kushiriki katika mikutano ya kawaida ya hadhara, katika mikutano ya kampeni za uchaguzi au shughuli nyingine yoyote ya chama chake, isipokuwa vikao vikuu vya maamuzi vya chama chake.