Mwenda wazimu_Ante
Member
- Apr 10, 2012
- 80
- 13
Ndugu wanaJF, huu ni mtazamo wangu lakini unaangalia kwa kina zaidi swala la katiba mpya ya serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania. Muungano maana yake ni kitu zaidi ya kimoja vinaungana kuwa kitu kimoja! Tanganyika na Zanzibar zimeungana lakini hamna ainisho sahihi la ni vipi vitu vya Tanganyika na ni vipi vile vya muungano. Ninapojaribu kufuatilia mijadala ya katiba kuhusu serikali zinazotakiwa kuwepo, haiingii akilini mwangu kwamba itawezekana kuendeleza usiri uliopo na aina ya muungano usiokua na uwazi uliopo kwa kuendelea kuwa na serikali mbili na pia haiingii akilini kama sisi wananchi masikini tunao uwezo wa kuzigharamia serikali tatu kwakuwa kama tutasema tuwe na serikali tatu itatubidi kuwa na muainisho wa vitu vya tanganyika eg Bank kuu, Bunge, mawaziri,katiba n.k na baadae tuwe na watu wengine wabunge, mawaziri, Bank n.k kwaajili ya muungano!!!! That is not affordable kwa nchi hii masikini...!!!!
Kwahiyo ninachoona ambacho kingefanyika kuongeza uwazi na uamuzi wa watanzania juu ya nchi yao sio kutafutia maoni kwamba ziwe serikali mbili au tatu bali ni kutafuta maoni kuwa muungano uendelee ama usiendelee! Baada ya hapo ndio suala la katiba ziwe mbili au tatu au kumi litakua na maana kwa wananchi..
Kero za muungano zitaibuka baada tu ya katiba mpya iwapo serikali haitachukua hatua. Vyama vya siasa Tanzania vinaonekana kuwa na woga na kuogopa kujitoa muhanga na kusema ukweli ambao ndio watanzania tunaoutaka kwa maendeleo ya taifa letu
Haya ni maoni yangu tu kama mtanzania....Nawasilisha
Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums