Katiba Mpya: Tulipo, Uzoefu Utumike - Katiba Ipo

Katiba Mpya: Tulipo, Uzoefu Utumike - Katiba Ipo

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Inajulikana kuwa katiba mpya inahitajika na wengi.

Wapongezwe Chadema kwa kuchukua jukumu la kuanzisha na kuratibu msukumo wa kurejelewa kwa mchakato huu muhimu wa kupatikana kwake.

Hatua hii isiyokuwa na chembe ya ubinafsi iliyojaa dalili zote za hatari, ni ya kupongezwa sana na kila mpenda haki, uhuru na usawa na hasa kila mzalendo.

Wapo watakaobeza hatua hii kwa kutokuelewa kwao au kwa kuwa ni wanufaika wa katiba iliyopo.

Wale wasioelewa ni jukumu letu kawaelimishe.

Hatuna haja ya kupoteza muda na wanufaika wa mfumo. Hao ni hatua muafaka sasa kuwasusia nyuzi zao na mabandiko yao yote.

Hatuna haja ya kuingia kwenye marumbano na watu hawa.

Tuwaache wapambane na hali zao.
 
Mie sinufaiki na lolote katika hio katiba maana ni kwa vile sifanyi uhalifu wala sijishughulishi na siasa! Siwezi kushabikia wala kupinga mchakato wa katiba mpya ila tu mtu asinishurutishe maana katiba hainiathiri kwa namna moja ama nyengine maisha yangu ya kawaida tu! Mnaopambania ipambanieni tu

Wenye maslahi ni wanasiasa na wahalifu maana ndio ina vipengele vya kuwatetea na kuwaneemesha kwahio lazma wawe na moto nayo!
 
Mstari ulioanza nao una kosa uhalisia. Raia wengi Tanzania hii hawana elimu ya kujua umuhimu wa katiba mpya. Mimi naelewa umuhimu wake na naunga mkono hoja hii lakini, ukweli lazima niuseme watanzania wengi hawajui chochote kuhusu katiba mpya ambavyo hawajui chohote kuhusu katiba iliyopo hivyo kuwafanya wasione umuhimu na wasiihitaji.

Kwa hiyo kabla ya yote.!! Public awareness inahitajika kwa nguvu zote. Lakini suala la hali duni ya kimaisha (vyuma kukaza) kumeongeza mlalo wa fikra za raia wengi kutohitaji katiba inayoitwa mpya...
 
Katiba ile ya Jaji Warioba ilipendekeza vipindi vya ubunge view vitatu tu. Ukiangalia sasa wabunge wetu wengi hawa ambao wameshatumikia vipindi viwili au vitatu hivi ni kweli wataweza kwenda kukubali kubadili Katiba hii iwe hivyo kweli kabisa!

Mwanagalie kama Waziri Mwigulu ambaye kwa vyovyote kwa sasa hawezi tena kufikiriwa kugombea URais mwaka 2025 - by huo mwaka atakuwa ametumika vipindi vitatu vya ubunge (Jimboni kwake wote ni bongolala hamna wa kumpinga) sasa hebu fikiria mtu kama Mwigulu aende kuwa kijiweni? Hivi ni kweli hiyo Katiba mpya inayofikiriwa kuwapa vipindi hivyo vya kutumikia ubunge itakubalika? Yangu macho!
 
Mie sinufaiki na lolote katika hio katiba maana ni kwa vile sifanyi uhalifu wala sijishughulishi na siasa! Siwezi kushabikia wala kupinga mchakato wa katiba mpya ila tu mtu asinishurutishe maana katiba hainiathiri kwa namna moja ama nyengine maisha yangu ya kawaida tu! Mnaopambania ipambanieni tu

Wenye maslahi ni wanasiasa na wahalifu maana ndio ina vipengele vya kuwatetea na kuwaneemesha kwahio lazma wawe na moto nayo!
Kama unadhani Katiba Mpya itakuletea ugali nyumbani unakosea, ila Katiba Mpya itatengeneza mazingira ya jumla kwenye nchi ambapo ukiwa na jambo lako utakwenda ofisi ya umma na kupewa msaada hitajika na wahudumu/wasimamizi bila kuwepo chenga chenga, wakileta ujuaji kwenye nafasi zao upo uwezekano ukiwaripoti mamlaka husika wakachukuliwa hatua stahiki badala ya kulindana kama ilivyo sasa.
 
Back
Top Bottom