Ambiente Guru
JF-Expert Member
- May 21, 2012
- 2,605
- 1,085
Katiba itamke wazi kuwa mgeni hatapewa uraia bila kujua Kiswahili.
Utaifa ni pamoja na kujua Kiswahili.
Wageni wanapewa uraia km njugu bila kujua mawasiliano, maadaili, tunu za taifa nk. kwa Kiswahili.
Familia ya Kihindi hapa Iringa, akina Maruaha – imekaa Tz miongo kadha lakini hawajui Kiswahili, aibu, ni raia wa Tz hawa.
Waende kwenye taasisi za Kiswahili wajifunze na kupewa vyeti vya lugha. Tasis /Waalimu zi/wamekaa bila kazi na wangeweza kupata kipato, tena dola kwa kusomesha wageni. Ni ajira kwa vijana wetu lukuki.
Kupata uraia Uingereza sharti ujue lugha yao kwa kufaulu mtihani. Huko Norway nako, pia sharti ukae miaka 7.
Maskini nchi yangu na mambo ya kirahisi rahisi!