Katiba mpya wanayoililia watu hasa wanasiasa tofauti itanisaidiaje mimi Mwananchi wa kijijini nisiyejihusisha na siasa?

Joined
Aug 8, 2017
Posts
72
Reaction score
84
Habari wana jukwaa.

Lengo Mimi ni Kuuliza tu...
Mm ni mwananchi wa kijijini huku ninayejishughulisha na Kilimo cha mazao ya biashara...

Hivi Hiyo katiba mpya wanayoililia watu Hasa wanasiasa mbalimbali itanisaidia nini Mimi mwananchi wa kijijini nisiyejihusisha na siasa!?
Umeme Upo, Maji yapo, na Huduma za Jamii nyingi zipo, uhitaji tu ni Walimu wachache kwenye shule zetu huku... Je katiba mpya itanisaidia nn kwenye kazi zangu hizi!?

Nimewasilisha Kama nilivyoulizwa, majibu yenu yanahitajika...
 
Itasaidia kuweka misingi imara ya nchi yako kwa nyanja ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Umetaja huduma za jamii tu yapo mengi zaidi. Ukijua faida ya katiba tuliyonayo utajua umuhimu wa katiba mpya maana faida zinazidiana i.e. alienunua 3000/= na kuuza kwa 5000/@)= ni tofauti na alinunua kwa bei hiyo na kuuza kwa 10000/=. Japo zote ni faida.
Asante!
 
Mtu unaweza kuingia JF halafu hujui faida za katiba. Je wale kule kijijini au mtaani inakuawaje sasa. Tanzania tuna tatizo kubwa sana la elimu kuliko tunavyo fikiria.
 
Siasa inatuathiri wote bila kujali unajihusisha nayo ama hujihusishi nayo. Hivyo bila kujali mlengo wako wa kisiasa ama upo neutral bado unaathirika na Siasa ndio maana umeuliza hii Habari ya Katiba.

Kwa lugha rahisi, SIASA SIO HOBBY

Nikuulize maswali
Zipo nchi huko duniani wameshamaliza hizo changamoto za umaskini, je uliwahi kusikia hawana Katiba ama hawabadili Katiba?

Umaskini wa nchi sio sababu ya kubadili katiba, CCM inatumia mtaji wa umaskini kama kigezo kwamba hata ikija katiba mpya haitaleta tofauti.
Pili, Katiba kama sheria mama lazima liende na wakati. Leo serikali inatunga sheria mpya kila mara kwa sababu maalum. Katiba nayo inahitajika kuangaliwa upya.

Tatu, unazijua haki zako za msingi?
 
Hivi kuna uhusiano kati ya uafrica/uesi na ujinga etii...!

Tuanzie hapa, unaelewa ni nini maana ya KATIBA??

Maana ata kujiita mtu, tena wa kijijini na kijiji chenyewe ni kwa mjibu wa sheria na KATIBA kama sheria mama.

Ukisema priority yako ni maji, elimu, makazi bora na afya ni kwa mjibu wa nini? Bila shaka jibu ni kwa mjibu wa sheria ambazo KATIBA ni sheria mama...! Hivi nani aliwaroga nyie people za black mpk akili....??? Mnyuuuuuhhhxxxx! Nyambafuu..
 
Nadhani ulienda shuleni kujifunza kusoma na kuandika. Kama umeweza ku register, ku sign in kwa user name yako na pssword. Basi unaweza ku google notisi za civics au elimu ya uraia mwema ili ujifunze maana ya katiba kimya kimya bila wa kuuona wazwazi ujinga wako ambao hata darasa la saba anayejitambua hana
 
Furaha yangu ni kwamba amepewa majibu bora kabisa. Ila hakuna aliyemwambia upumbavu unaomsibu. Huyu ni kati ya wale wanawabeza wanaodai marekebisho ya katiba au katiba mpya. Wanatakiwa kujua kuwa ni katiba iliyowaingiza madarakani na ubora wa katiba ni msingi imara kabisa kwa ustawi wa taifa lolote. Tuache mzaha, tudai katiba mpya na mara zote tuwe majasiri wa kuitetea katiba yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…